January 19, 2018

Dalili za kwanza za mwanamke kuwa na mimba ni zipi?

Karibu katika blog yetu ta timheaven.com, tunazo makala nyingi ambazo zitajibu maswali yako mengi kuhusiana na swala zima la mimba, kwanzia siku ya kwanza mpaka utakapo jifungua, Bofya hapa kutazama makala nyingi zaidi

Moja kwa moja kwenye mada yetu. Dalili kuu na iliyowazi kuliko zote ni kukosa hedhi. Mwanamke akiwa katika harakati za kutafuta mtoto (kupata mimba) ama akifanya mapenzi bila kutumia kinga yoyote na akajikuta hapati hedhi katika muda unaotakiwa, mara nyingi hii ina maana kwamba amepata mimba.

Isikupite hii: Mahusiano kati ya Ute wa mwanamke na kubeba mimba. (Ute wa mimba)

Dalili nyingine ni pamoja na kuvimba matiti na chuchu kuchomachoma. Baadhi ya wanawake wanaota nywele nyingi sehemu za siri (mavuzi) na wengine wengi rangi ya chuchu zao iinabadilika kuwa nyeusi.

Pia, karibu nusu ya wanawake wajawazito huumwa tumbo na wengine hutapika. Wanawake wengi husikia mkojo mara kwa mara na wengine hujisikia wachovu na kuona kizunguzungu, hasa katika miezi mitatu ya mwanzo.

Wakati mwingine wanawake hupenda au huchukia baadhi ya vyakula, kichefuchecfu n.k. Ili mwanamke awe na uhakika kama ni mjamzito au hapana, akapimwe mkojo kwenye kliniki au hospitalini, mara anapokuwa na wasiwasi.