January 15, 2018

Faida za ubuyu kwa afya yako

Mungu ameumba miti na mimea kwa ajili ya binadamu. Kila mti au mmea una makusudio yake. Mbuyu ni miongoni mwa miti yenye faida nyingi na maajabu mengi. Vitu vyote vilivyomo kwenye mbuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu.
Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine yoyote unayoyajua.

1. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.

2. Ubuyu una kiwango kingi cha madini ya Kalisiamu (Calcium) mara 2 zaidi ya maziwa ya ng’ombe, pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja na madini ya Chuma, Magineziamu na Potasiamu ambayo ni mara 6 zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi!

3. Husaidia kujenga neva za fahamu mwilini.

4. Ina virutubisho vya kulinda mwili.

5. Ubuyu una vitamini B3 na B2 ambayo ni mhimu katika kuondoa sumu mwilini na umeng’enyaji wa madini ya chuma, kimsingi vyakula vyenye afya zaidi kwa ajili ya mwili ya binadamu huwa pia huwa na vitamin B2.

6. Unaongeza kinga ya mwili sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C

7. Huongeza nuru ya macho

8. Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika

9. Ina magnesia ambayo husaidia kujenga mifupa na meno

10. Husaidia wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya figo