January 2, 2018

Historia fupi ya maisha ya Ali kiba.

Ali Saleh Kiba a.k.a King Kiba; anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Ali Kiba. Alizaliwa Novemba 29 1986, ni mwanamuziki wa Tanzania, mwimbaji na mtunzi wa nyimbo chini ya lebo ya Rockstar4000.

Ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia ya watoto wanne, ambaye mdogo wake pia ni mwanamuziki wa Kitanzania. Ali saleh ni mwimbaji mwenye kipaji chenye tofauti na wasanii wenzake.

Mwaka 2011, Ali Kiba alichaguliwa kama msanii wa bora wa Afrika Mashariki" - Tanzania, Kenya na Uganda. Kwa mwaka 2015 alishinda tuzo tano za Kili awards. Tarehe 20 Mei 2016, kampuni ya kimataifa inayojishughulisha na muziki Sony Music Entertainment ilitangaza kumsainisha mkataba wa kufanya kazi na Ali Kiba.

Pia ni mshindi wa tuzo mbalimbali za kimataifa kama vile MTV n.k