January 1, 2018

Historia fupi ya zari the boss lady (zarinah hassan).

Alizaliwa 23 Septemba 1980. Jina lake halisi ni Zarinah Hassan (Zari). Alikulia katika mji wa Jinja nchini Uganda. Alisoma elimu yake ya awali katika eneo hilo na kujiunga na Shule ya Wasichana ya Jinja na baada ya hapo alikwenda katika Mji Mkuu wa Uganda, Kampala ambapo alikuwa akiimba katika matamasha mbalimbali aliyokuwa akihudhuria na baadae alikwenda nchini Uingereza (London) alikopata stashahada ya masuala ya urembo katika chuo cha cosmetology.

Babu yake kwa upande wa mama wana asili ya India na bibi yake ana asili ya Uganda. Babu yake kwa upande wa baba ana asili ya Somali wakati bibi yake ana asili ya Burundi.
Historia yake ya muziki.
Zari alizanza masuala ya kuimba mapema akiwa shule ya msingi ambapo alikuwa akitumbuiza katika matamasha yaliyoandaliwa shule hapo na amshindano mengine nje ya shule. Alipojiunga sekondari alijiunga na kundi la muziki lililomsidia kushinda shindalo la muigizaji bora wa kike mara mbili mfululizo. Baada ya kufanya vizuri zaidi katika masuala ya muziki, alipumzika kidogo alipotoka Uganda na kwenda Uingereza kusoma japo alitamani kuendelea kuimba.

Zari anaamini kuwa maisha yake ya kimuziki yalianza kupata mafanikio mwaka 2007 alipotoa wimbo wake wa kwanza uliokwenda kwa jina la oliwange (wewe ni wangu). Video ya wimbo huo ulifanikiwa kuingia kwenye tuzo za Channel O katika kipengele cha Video Bora ya Mwaka kutoka Afrika Mashariki.

Mwaka 2008 alishinda Tuzo ya Channel O katika kipengelea cha Mwanamuziki Bora wa Afrika Mashariki. Mwaka 2009 alishinda tuzo ya Mrembo Bora wa Mwaka katika kipengele cha wanaoishi nje ya nchi.

Familia.

Zari ana watoto wanne, Pinto, Didy, Quincy, Nillan na Tiffah. Kwa sasa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki mashuhuru wa Tanzania Nasib Abdul, maarufu Diamond Platnumz. Taarifa kutoka kwa Diamond Platnumz zimeeleza kuwa mrembo huyo ni mjamzito na siku za usoni atajifungua mtoto wa kiume.
Biashara.
Zari anaishi nchini Afrika Kusini ambapo anafanya biashara zake. Anamiliki Chuo (tertiary college) na pia duka la urembo katika mji mkuu wa nchi hiyo Pretoria lakini pia anafanya shughuli zake za muziki.