January 6, 2018

Hizi ndio bank 5 zilizofutiwa leseni na BOT.

Benki kuu (BoT) imezifutia leseni benki tano (5) kwa kutokuwa na mtaji wa kutosha kujiendesha na hivyo kuweka hatarini amana za wateja wao na usalama wa sekta ya fedha nchini.

Benki hizo ni :

1.Covenant Bank For Women (T) Ltd
2.Efatha Bank
3.Njombe Community Bank
4.Kagera Farmer's Cooperative Bank
5.Meru Community Bank

Benki hizo zitakabidhiwa kwa mfilisi ambaye ni Deposit Insurance Board na kuruhusu utaratibu wa kisheria uendelee.