January 11, 2018

Mambo 4 hupaswi kufanya wakati unapoingia kwenye mahusiano mapya.

1. Kulinganisha mahusiano.
Hakuna siku hata moja ambayo mahusiano yatakuja kufanana. Unapoamua kuanza mahusiano kamwe usijaribu kumlinganisha mpenzi wako wa sasa na yule wa kale. Fitzgerald aliwahi kusema "kuna aina nyingi za upendo duniani lakini uwezi kupata upendo mmoja mara mbili". Hatuwezi kutafuta mambo ya kale kwenye jambo jipya, kwa hivyo epuka tabia hii kabla haijaanza.

2. Usije na mpenzi wako wa zamani (Ex)
Kila mtu anayekuja katika maisha yetu, hubaki ndani yetu kwa namna moja ama nyingine. Unapokuja wakati wa kusonga mbele, yaliyopita lazima yabaki nyuma. Mara nyingi tunapokuwa kwenye mahusiano mapya huwa tunajikuta tukiongea kuhusu wapenzi wetu wa zamani, huwa inatokea tu na wote hatujui inatokeaje. Tunapoongea kuhusu mahusiano yetu ya kale ndani ya mahusiano yetu mapya tunajifunga na kutuzuia kujua mambo mapya katika mahusiano. Tumia muda wako kujenga mahusiano yako na siyo kuongea kuhusu mpenzi wako wa zamani.

3. Mchepuko.
Huwezi kujenga mahusiano mapya ama ambayo huko sasa hivi kama bado unamichepuko. Michepuko ni dalili ya uchanga kwenye akili ya mtu, waache watoto wa miaka 15 wachepuke sio wewe mtu mzima ambaye unakaribia kuoa. Umeisha kuwa mtu mzima ni wakati wa kujenga maisha yako ya sasa na baadaye. 

4. Nitakuwa mtu yeyote unayetaka niwe.

Mahusiano hayalazimishwi.  unapojaribu kujibadilisha ni kama kulazimisha kitu ambacho hakipo kiwepo. Ilinde asili yako, hasa kama ni njema. Usifanye vitu ambavyo sio asili yako na vinapingana na maadili eti kisha mpenzi wako mpya anapenda. Be you and who you are. At the end of the day, you have to be conscious of yourself, no one else.