January 5, 2018

Mambo ambayo mwaka 2017 umenifunza kuhusu mahusiano na ndoa.

1. Mwanaume kuna aina fulani ya wanawake kwa namna yoyote ile unatakiwa uwaepuke. Wanawake wanaodhani uzuri wao ni zaidi kuliko tabia zao.

2. Mwanamke Tafuta mwanaume atakaekuongoza na kumtumikia Mungu, sio yule atakaekimbilia kutaka ngono pekee.

3. Mwanaume Usimpe MIMBA mwanamke kabla hujamfanya kuwa mkeo wa halali.

4. Mwanamke usikubali MIMBA ikufanye kuwa SINGLE MOTHER, kabla ndoa haijakufanya kuwa MKE HALALI.

5. Mwanaume Unapokua na bidii ya kumtafuta Mungu kama utavyutavyo wanawake, Mungu atakupa mwanamke ambae wala hutahangaika kumtafuta.

6. Mwanamke, Wanaume bora sio kwamba hawapo, wapo ila ni tabu mno kuwavutia. Wanamuda na majira yao. Wanazo quality za wanawake wanaowahitaji na Muda wao wakuoa ukifika huoa tu pasina external pressure.

7. Mwanaume, Usimuite mwanamke ni CHEAP kwa vile amekukubali kirahisi, anakunyenyekea na kukutii. Mwanamke huyo huyo ni mgumu kwa wanaume wengine

8. Kama unampenda mtu, mwambie wazi na mpe uhakika (clarity) na kama haumpendi, mueleze wazi ajue. Binadamu tupo nyuma ya wakati. Usimpotezee mtu muda.

9. Mke au mume wako anaweza kukusaliti, ila Mungu hawezi kukusaliti kamwe. Mtangulize Mungu kwa kila hatua unayopiga.

10. Ofcourse mwanaume/mwanamke anaweza akakuacha tena kwa dharau nyingi, ila endapo utaijua thamani yako hutateteleka kamwe. Utajikuta umemuacha aende tu!

11. Owa/olewa na mtu ambae anaweza kukuombea na sio kufanya mapenzi pekee!

12. Kwa mwanamke bora, haitajalisha ni kiasi gani cha pesa ulichompa, suala la muhimu ni muda uliowekeza kwake. TIME invested is the real measure of love.

13. Kama ukimuuliza Mwenyezi Mungu, sheria ya smart dating ni ipi? Jibu ni rahisi tu. "Usimvue mwanamke Nguo kabla hujamvalisha pete ya ndoa"

14. Mwanamke, kama ukimuuliza Mungu mwanaume bora yukoje na nitajuaje kama ananipenda? Jibu ni rahisi. "Kama mwanaume huyo hana hofu ya Mungu ni vema ukajiandaa na lolote. Mwanaume asiye na Mungu hawezi kukuongoza kama KRISTO alivyoliongoza kanisa lake.

15. Tafuta mwanamke ambae atachangamsha akili yako, sio ambae atakuchangamsha kingono pekee.

16. Watu walio perfect hawapo kabisa, ila watu bora wapo kila mahala.

17.Matokeo ya kuwadharau wanaume walio bora na ku-hang out na wavulana wenye swagga, ni kuja kuwa na uchungu na mwanafalsafa bora ukiwakandia wanaume pale umri utakavyokua umeenda na usione future yoyote ile ktk maisha yako.

18. Hakuna mwanamke mpumbavu kama yule anaemdharau mwanaume kutoka na hali yake ya umasikini aliyonayo sasa. Kila mwanaume mwenye bidii ni tajiri aliyeko katika kipindi cha mpito.

19. Mume ni vema awekeze kwa mkewe, sio mali pekee, bali uaminifu, upendo, na intimacy. Uwekezaji kwa mke una matokeo chanya, ila uwekezaji kwa michepuko ni kufilisika kiakili na kiuchumi.

20. Baadhi ya wale tunaowaita wapenzi wapo katika maisha yetu ili kutuharibia malengo yetu. Shetani anakuja kama girlfriend akihitaji kukumaliza kiakili na kiuchumi na vilevile anakuja kama boyfriend akihitaji sex pekee wala sio ndoa wala malengo au maono yoyote yale. Hivyo kuwa makini.