January 10, 2018

Mambo unayopaswa kuyaacha ili uondokane na adha ya umaskini!

Watu wengi wanashindwa kufanikiwa au kufikia mafanikio yao bila wao kujua tatizo ni nini, imekuwa kama ugonjwa kwa watu wengi kuendelea kulalamikia serikali au wazazi wao kama chanzo na sababu ya kushidwa kwao, na wengine wamekuwa wakikata tamaa kabisa ya mafanikio yao bila wao kujua kinachokwamisha ubora wa maisha yao.

Leo tutajifunza pamoja vikwazo vya mafanikio ambapo kama utavifanyia kazi basi utaanza kushuhudia mabadiliko chanya maishani mwako, kumbuka kuwa hakuna aliyezaliwa kuwa masikini. Ungana nasi.

1. KUKOSA USHAWISHI BINAFSI.
Watu wengi wanashindwa kufanikiwa katika maisha yao kwa sababu ya kukosa msukumo binafsi. Rafiki yangu, hakuna mtu yeyote ambae atakaa chini na kupanga maisha yako au kuna mtu ataacha shughuli zake kwaajili ya kupigania maisha yako, wewe ndiye unayejua ugumu na uchungu wa maisha yako!! Amka sasa kuwa na msukumo kutoka moyoni mwako wa kushinda, usisubiri mtu fulani aje akuambie nenda kazini au fanyabiashara. Wewe mwenyewe kaa chini jitume utafanikiwa.

2. UOGA
Hiki ni kikwazo kikubwa sana kwa watu wengi katika kuyafikia mafanikio yao, watu wengi wamekuwa masikini na wengine kufa masikini kwasababu ya uoga, hasa uoga wa kukataliwa na uoga wa kushindwa, kama unataka kufanikiwa katika kila kitu maishani mwako usiogope kuomba au kusema chochote mbele ya watu eti kwa kuogopa kukataliwa! Rafiki usiusemee moyo wa mwenzio, usiogope!! lakini pia usiogope kushindwa yani mtu anataka kufanyabiashara lakini kitu cha kwanza anawaza ni kushindwa anaamini kuwa yeye hawezi na akianzisha atafeli.

3. KUTOKUJIAMINI
Watu wengi sana wanakosa kujiamini wenyewe. Msomaji wetu hebu jiamini kuwa wewe unaweza. Amini kuwa ndani yako kuna mtu mkubwa saana na anayeweza kufanya vitu vikubwa pia, Acha kusikiliza watu wengine wanasema nini kuhusu wewe, Usikilize moyo wako unasema nini kuhusu wewe, Usikubali kushindwa!! Thubutu kwa kila jambo unaloambiwa lenye mafanikio na usiamini kuwa huwezi. Na zaidi ya yote usikubali kuogopeshwa na watu wengine. Wapo watu watakuvunja moyo na kukuambia eti ndoto yako ni kubwa sana na kwamba hutaweza kuifikia. Wapuuzie watu wa namna hiyo na utumie maneno yao kama kichocheo cha wewe kutafuta kufanikiwa zaidi na zaidi.

4. KUKOSA LENGO
Rafiki, malengo yako nini? Lengo ni ndoto zenye mipaka. Kuna Malengo ya Muda Mfupi, Malengo ya Muda wa Kati na Malengo ya muda mrefu. Jewewe malengo yako ni yapi?

Lazima ufahamu kuwa, huwezi kufanikiwa katika maisha yako kama huna malengo ya maisha yako!! Kama huna malengo, basi panga leo. Yaandike malengo yako. Mtu asiye na malengo ni sawa na mtu ambae anaenda stendi kupanda gari lakini hajui anaenda wapi, atapanda gari gani na atashukia wapi!!! Huyu mtu hatofika popote bali atazunguuka na gari hadi usiku gari linapokwenda kupaki basi litamshusha popote. Tambua Malengo yako na kamwe usiwe mtu wa BORA LIENDE.

5. KUTOKUWA MAKINI NA MUDA
Watu wengi wanaposikia muda ni mali huwa hawaamini leo nataka ujue uhusiano uliopo baina ya muda wako na umasikini wako au utajiri wako.

Unatumiaje muda wako ambao unatoka kazini? unatumiaje muda wako baada ya shughuli za masomo chuni au shuleni? wewe mama wa nyumbani unatumiaje muda wako ambao unakuwa hauna kazi nyumbani? hapa ndipo kasheshe na umasikini wa watu ulipo.

Kila sekunde na saa inayopita lazima uhakikishe unafanya kitu chenye manufaa na muunganiko wa moja kwa moja na ndoto zako, mfano ukitumia masaa mawili unajifunza kitu chenye mafanikio kwenye maisha yako basi unayavuta mafanikio yako masaa mawili kama mafanikio yako yalikuwa uyafikie kwa siku mbili na masaa mawili basi utakuwa umebakiza siku mbili.

Kama unatumia muda wako kuangalia TV, kupiga umbea, kupiga story zisizokuwa na maana ukifanya hivyo masaa mawili kwa siku ndani ya mwaka utakuwa umepoteza zaidi ya miezi 4, basi hiyo miezi minne ndio umesogeza mbele mafanikio yako. Kwaiyo kama ungetakiwa ufanikiwe kwa miaka miwili basi utafanikiwa kwa miaka miwili na miezi minne.

6. KUKOSA BIDII NA NIDHAMU YA KAZI
Kujitoa limekuwa tatizo kwa watu wengi sana, na linawakwamisha watu wengi sana kuyafikia mafanikio yao.

Mara nyingi watu wanafanya mambo yao kwa mazoea, uzembe na uvivu uliokithiri. Kamwe huwezi kufanikiwa kwa kufanya kitu kile kile kwa njia ileile, juhudi na mbinu zilezile na utegemee kufanikiwa!!

Rafiki yangu ili ufanikiwe nilazima ujitume kikamilifu kwa kujitoa na kuwekeza nguvu, muda na maarifa yako kwenye shughuli zako, iwe ni kazi ya kuajiriwa, biashara nk. ndipo utakapoona mafanikio yoyote. Acha uvivu, uzembe na kufanya mambo kwa mazoea, Jitoe, Jitume, Pambana na utafanikiwa.

7. KUPUUZIA NIDHAMU YA MATUMIZI YA MUDA
Tafiti zinaonesha kuwa watu wengi hupoteza zaidi ya miezi 9 kila mwaka, ndani ya miaka 15 tayari watu husogeza mbele mafanikio yao kwa zaidi ya miaka kumi. kwa hiyo ukichukuwa miaka kumi ya kutafuta maisha na ile miaka kumi aliopoteza ni miaka 20.

Kwa mfano ameanzakutafuta maisha na akiwa na miaka 30-40 miaka ya kufikia mafanikio yake itakua 50 na maisha now ni mafupi hayafiki huko na kipindi anaendelea kutafuta anapoteza tena masaa kadhaa. lazima ufe masikini. amka sasa mtanzania acha kutumia muda wako vibaya kwani muda wako unaoupoteza sasa utakugharimu.