January 28, 2018

Maneno 30 ya hekima kwa maisha ya kila siku.

Hekima ni hali ya mtu anapopata ujuzi wa kudadisi, kuchanganua, kuelewa na kutenda au kusema kwa njia nzuri naya kukubalika na wengi. Maneno ya helima hutokana na tajiriba ya mtu, umri au ujuzi katika fani fulani, maisha, taaaluma, biashara au kazi.

Ujuzi huu humwezesha mtu kutegemewa kwa mawaidha au muongozo na wanaojifunza anu wnaotaka kobobea wakimwiga youle mwenye maneno ya hekima.

Maneno mengine ya hekima yanakuwa katika semi za watu wa zamani wanaojulikana kama wahenga au wenye hekima wa zama za kale. Hapa pana baadhi ya maneno ya hekima yanayojulikana.

1. Maisha ni kile kinachokutatiza wakati unapangilia mikakati yako
Watu hujulikana maisha yao kwa masaibu yanayowapata na baadaye suluhisho ila si kwa wakati wao wa furaha.

2. Maisha ni asilimia kumi ya kile kinachonipata na asilimia tisini ni kile nikifanyacho katika kukabiliana na hiyo hali
Wakati mwingi unaotumia maishani ni unapotafuta suluhu ya mambo yaliyokupata na muda mfupi ni ule ambao jambo mpya linafanyika maishani mwako.

3. Muda wako unakikomo, kamwe usipotee kwa kujaribu kuishi maisha ya mtu mwingine
Ina maana kuwa unafaa kuishi maisha yako mwenyewe ila si kujaribu kuwa kama watu wengine kwani muda unaoishi duniani una mwisho.

4. Maisha huchanua na kusinyaa kutokana na ujarisi wa mtu husika
Waweza kufurahishwa, kufunzwa au kukasirishwa na maisha yako kulingana na inavyoyaishi na kulingana pia na mtazamo wako wa mambo yanayokupata maishani.

5. Enenda wima katika ndoto zako,na utaishi maisha uliotarajia
Ukiishi maisha yako ukifuata ndoto zako utaishi maisha ambayo utapendezwa nayo kwani mwishowe ndoto zako zitatimia ukitia bidii. Kama tujuavyo watu huangali mwisho wa safari bali si mwanzo wa safari.

6. Maisha hayapimwi kwa idadi ya pumzi tuivutayo, hupimwa kwa idadi za hatua zichuako pumzi zetu
Katika maisha yako jaribu kufanya mambo mengi yatakayo badili watu ili ukumbukwe kwani mambo ambayo unayafanya kumsaidia mwenzako ni yayo unazoacha duniani.

7. Changamoto hupendeza maisha,na kukabiliana nazo ndio maana halisi ya maisha.
Matatizo unayoyapata kila siku na mbinu unazotumia kutafuta suluhuisho ndio maisha yako. Hivi basi inafaa uwe na mtazamo mzuri unapopatwa na majaribu.

8. Mtu hata badili maisha yake kama hakuanza na kubadili fikira zake
Kama unataka kubadilisha maisha yako yawe mazuri unafaa kuanza kwa kubadili mtazamo wako wa jambo lolote maishani.

9. Kila wakati kabla ya kufikiria vitu ambavyo hauna chukua muda wa kuwaza vitu ambavyo unavyo
Ni vyema kuwa na mtazamo chanya maishani hivi basi usinugunike kwa vitu ambavyo hauna bali ushukuru Mola kwa vitu ambavyo amekupa.

10. Maisha ni kile ukitendacho,ipo hivyo itakuwa
Matendo yako ndiyo yanayoonyesha wewe ni mtu wa aina gani, kwa hivyo kwa kila kitu unachofanya hakikisha unaonyesha kuwa wewe ni mtu wa aina nzuri

11. Kabla ya kutenda jambo lolote fikiria ambavyo jambo hilo litaadhiri maisha yako
Ina maana kuwa kabla ya kutenda jambo lolote unafaa kufikiri kama ungalitendewa ungaliskia aje? Kwa mfano; kabla ya kusema mabaya kuhusu mwenzako ni vyema kufikiria ‘mtu angalisema mabaya kukuhusu ungalifurahi?

12. Msinihukumu kwa mafanikio yangu, nihukumuni kwa mara ngapi nilianguka na kuinuka tena.
Usitumie mafanikio ya mtu yeyote kujua maisha yake bali angalia matatizo aliyopitia na suluhu alizopata kufika mahali alipo.

13. Mimi si mtakatifu, labda ukimfikiria mtakatifu kuwa mwenye dhambi asiyeacha kujitahidi
Hakuna mtu asiye na dhambi maishani lakini kuna watu wa aina mbili, wanojitahidi kutofanya dhambi na wasiojali kama wanatenda dhambi

14. Chuki hufunga akili. Inazuia ubunifu wowote wa mbinu. Viongozi hawana nafasi ya kuchukia.
Ina maana kuwa tunafaa kupendanda ili kuendelea maishani hasa viongozi. Kwa mfano; kama kiongozi wa taifa anawachukia watu katika nchi yake hatakubali kufanya kazi nao ingawa kazi hio itasaidia kuendeleza taifa lake.

15. Kama wanaweza kujifunza kuchukia, basi wanaweza kufundishwa kupenda, kwa sababu kwa kawaida ni asili yake upendo kuja kwa moyo wa mwanadamu kuliko kinyume chake
Ni heri kuwapenda wenzako kuliko kuwachukia kwani upendo ndio hufaidi ila si chuki.

16. Hakuna aliyezaliwa awe na chuki
Kila mmoja huzaliwa na sababu ya kuwa duniani na hakuna anayezaliwa kwa sababu isiyofaa wengine.

17. Watu wenye ujasiri hawaogopi kusamehe kwa ajili ya amani
Ina maana chuki huchosha moyo kwa hivyo heri kusamehe wanaokukosea maishani.

18. Utafanikiwa kwa mengi katika dunia hii kupitia matendo ya rehema kuliko kwa matendo ya kuadhibu watu
Tunafaa sote kufanya mambo mazuri kwa wengine kwani matendo mazuri hufaidi zaidi kuliko matendo mabaya

19. Ongoza kutokea nyuma -na wafanye wengine waamini wao ndio wako mbele.
Si vyema kujionyesha kuwa mwenye hekima kuliko wengine, heri kusikiliza wengine mara kwa mara

20. Ninapinga ubaguzi wa rangi kwa sababu ninauchukulia kuwa jambo la kipuuzi, iwe linatoka kwa mtu mweusi au mweupe.
Watu wote ni sawa wawe walemavu au tofauti nasi sote tuko sawa

21. Mara zote huonekana haliwezekani mpaka lifanikiwe.
Jambo huonekana kuwa ngumu kabla ulifanye lakini baada ya kulifanya watu hushangazwa na urahisi wa jambo hilo.

22. Mtu mwenye akili si yule anayejisikia kuogopa, bali yule aushindaye woga.
Woga hausaidii kwani woga hufanya mtu asifanye jambo ambalo huleta mafanikio baadaye kwa hivyo heri kuondoa woga maishani

23. Heshima ni kwa wale wasioupa mgongo ukweli, hata pale mambo yanapoonekana kufunikwa na giza na kutokufurahisha
Ni vyema kuishi maisha na ujasiri katika lolote unachofanya hata kama hujui matokeo yake kwani imani yako kwa jambo flani ndio hufanya jambo hilo kutendeka.

24. Kwa sababu kuwa huru si tu kutupa minyororo, bali kuishi katika namna inayoheshimu na kukuza uhuru wa wengine.
Hakikisha kuwa maisha yako na mienend yako inaonyesha kuwa uhuru wako una faida duniani

25. Elimu ni silaha yenye nguvu kuliko zote unayoweza kuitumia kubadilisha dunia.
Ina maana kuwa elimu husaidia kubadilisha mtu binafsi na baadaye dunia husaidika

26. Mtu anapofanya kile anachokiona kuwa wajibu wake kwa watu wake na nchi yake, mtu huyo anaweza kupumzika kwa amani
Kila mara unapofanya kitu kizuri moyo wako hua na amani kwa hivyo jaribu kufanya mambo mazuri mara kwa mara.

27. Kumbuka, kama unaelekea njia mbaya, Mungu huruhusu kugeuka kwa yeyote
Hujachelewa kufanya mazuri maishani kwani waeza geuza maisha yako wakati wowote na kuishi vizuri.

28. Mtu haezi enda njia mbaya usipomwacha aeende pia haezi enda njia nzuri usipomwacha aende.
Wakati mwingine ni vyema kumwacha mwenzako afanye apendacho ili aweze kuelimika kwa makosa yake kwani ukimweleza kuna uwezekana hatakuamini

29.Kuna wakati wa kuondoka ata wakati ambapo hakuna pahali pa kuenda
Usikubali kuishi kupoteza muda wako maishani kwani muda unayoyoma.

30. Kuna matatizo machache katika mambo tunayoogopa kuliko mambo tunayootamani
Familia muhimu ni kama viazi, mizizi inapatikana chini
Familia nyingi zinazoongoza hua na viongozi wema katika vizazi vilivyo pita. Kwa hivyo unaweza kutengeneza maisha ya vizazi vitakavyo kufuata wakati huu.