January 3, 2018

Maneno ya Madam Flora kwenye picha yake na mume wake Mr. Daudi

Kwa mwaka 2017 tumeona mastaa wengi wakifunga ndoa, ukizungumzia ishu ya kufunga ndoa huwezi kuacha kumtaja Madam Flora ambae wengi wamemzoea kwa jina la Flora Mbasha ambaye ni mwimbaji wa Gospel jina la Mbasha limezooeleka kwasababu ya mume wake wa zamani Emmanuel Mbasha lakini kwa sasa anafahamika kama Madam Flora. 
Kupitia instagram account ya Madam flora ameamua kuelezea jinsi mwaka wa 2017 ulivyokuwa mwema kwake baada ya kupata nafasi ya kuolewa kwa mara ya pili na mume wake Daudi Kusekwa
 “Ahsante Mungu maana 2017 ulikuwa ni mwaka wa furaha kwangu, ahsante mume wangu mpenzi @daudikusekwa13 kwa kunifanya nitabasamu wakati wote, naamini 2018 utakuwa ni wa baraka zaidi.” – Madam Flora 

“Mungu akuzidishie hekima, busara na maarifa ili tufanikiwe zaidi, kicheko kisipungue ndani ya nyumba yetu. Neema ya bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu baba na ushirika wa Roho mtakatifu ukae nasi siku zote sasa na hata milele amina” - Madam Flora 
“Hivi ndivyo tulivyomaliza 2017 na kuanza 2018, tunamshukuru sana Mungu kwa kutuvusha salama. Tunaamini kipo kicheko zaidi kwa mwaka huu kwani ni mwaka wa mafanikio makubwa na tumeuanza vyema. Tunamrudishia Mungu heshima, sifa na utukufu, kwani bila yeye tusingefika hapa tulipo leo” -Madam Flora