January 24, 2018

Misemo 100 kuhusu maisha.

Misemo mia moja ya maisha ya watu wenye ushawishi mkubwa kama Albert Einstein, Benjamin
Franklin, Bill Gates, Leonardo da Vinci, Pablo Picasso, Voltaire ama William Shakespeare.

Maisha nikama kuendesha baisikeli. Ukitaka kuweka msawazo lazima uendelee kusonga

Kaa katika uzuri wa maisha. Tazama nyota, na ujione ukikimbia nazo. - Marcus Aurelius

Furaha yako maishani inategemea na ubora wa mawazo yako - Marcus Aurelius

Maisha yetu yako kuligana na mawazo yetu - Marcus Aurelius

Mambo madogo yanahitajika kufanya maisha mema; yote ni ndani ya wewe mwenyewe katika njia yako ya kufikiri - Marcus Aurelius

Sio heshima tu kuishi maisha ukifanya makosa, lakini ni muhimu zaidi kuliko kuishi maisha bila kufanya chochote - George Bernard Shaw

Maisha si juu ya kujitafuta kibinafsi . Maisha ni kujijenga mwenyewe. - George Bernard

Wale sioweza kubadili mawazo yao hawawezi badili chochote - George Bernard Shaw

Ishi nikama wafa kesho. Jifunze nikama utaishi milele - Mahatma Gandhi

Panapo upendo pana maisha - Mahatma Gandhi

Pale unapo jiamini, ndipo unapojua kuishi - Johann Wolfgang von Goethe

Maisha ni mali ya wanaoishi, na anayeishi lazima awe tayari kwa ajili ya mabadiliko - Johann Wolfgang von Goethe

Kama ushawahi kula ukilia, haujui utamu wa maisha - Johann Wolfgang von Goethe

Hakuna kitu cha kutisha kuliko kupuuza katika hatua - Johann Wolfgang von Goethe

Kuishi ni mara moja pekee, lakini ukifanya vema, mara moja yatosha - Mae West

Hamna utamu kwa kupatikana ukicheza kwa udogo-kwa kukubali maisha duni kuliko yale uko na uwezo wa kuishi. - Nelson Mandela

Mtu akinyimwa haki ya kuishi maisha anayokusudia, hana budi ila kuwa mhalifu - Nelson Mandela

Kawaida huonekana haiwezekani hadi inapofanyika – Nelson Mandela

Waandani wazuri, vitabu vizuri, na dhamiri ya usingizi: hiyo ndio maisha bora - Mark Twain

Uoga wa kifo hufuatia uoga wa maisha. Mtu anayeishi kikamilifu ako tayari kufa wakati wowote - Mark Twain

Kwa maneno matatu naweza jumlisha kila kitu nimejifunza kuhusu maisha: Na yaendelea - Robert Frost

Maana ya maisha ni kupata kipawa chako. Jukumu la maisha ni kuipeana - Pablo Picasso

Ningetaka kuishi kama mtu maskini nikiwa na pesa nyingi – Pablo Picasso
Twaweza msamehe mtoto kwa kuogopa giza; janga la maisha ni wakati wazee wanaogopa mwanga: Plato
Lazima ufahamu maisha kwa ujumla, sio tu kipande kidogo tu. Hio ndio sababu lazima usome, hio ndio sababu lazima utizame angani, hio ndio sababu lazima uibe, na ucheze, na uandike mashahiri, na usononeke, na uelewe, kwa hayo ndio maisha. Jiddu Krishnamurti
Ni ukweli unaookoa, sio juhudi yako ya kuwa huru- Jiddu Krishnamurti
Mtu haogopi yasiotambulika; mtu huogopa yanayojulikana kufikia mwisho- Jiddu Krishnamurti
Wewe ndiye mkuu wa hatma yako. Unaweza athiri, elekeza na kudhibiti mazingira yako mwenyewe. Unaweza fanya maisha yako vile wataka yawe. – Napoleon Hill
Kabla mafinikio yaje kwa maisha ya mwanamme, yeye yuko na uhakika wa kupatana na pigo la muda na hata kushindwa- Napoleon Hill
Aliye na kwa nini ya kuishi anaweza stahimili kwa vyovyote. Fredrich Nietzsche
Siri kubwa la maisha yenye mafanikio ni kutafuta hatima yako ya kufanya, na kuifanya. Henry Ford
Unapofikiri unaweza, ama hufikiri huwezi- uko sawa – Henry Ford
Hesabu umri wako kwa marafiki, sio miaka. Hesabumaisha yako kwa tabasamu, sio machozi- John Lennon
Ndoto unayoota peke yako ni ndoto tu. Ndoto uotayo pamoja ni ya ukweli. Johns Lennon
Maishani, tofauti na mchezo wa chess, mchezo waendelea baada ya kumaliza- Isaac Asimov
Kitu cha huzuni kwa maisha sasa ni kwamba sayansi yapata maarifa haraka kuliko jamii inavyo pata busara. Isaac Asimov
Maisha ni mazuri. Kifo ni Amani. Kinachosumbua ni mpito. Isaac Asimov
Mtu anayethubutu kupoteza lisaa limoja hajatambua thamani ya maisha- Charles Darwin
Kama vile siku ulivyoishi vizuri huleta usingizi mzuri, pia maisha ulivyoyaishi vzuri huleta kifo. – Leonardo da Vinci
Napenda wale wanaoweza kutabasamu kwa shida. – Leonardo da Vinci

Namna nyingi, ucheshi wote, urembo wote wa maisha hujumuishwa na mwanga na kivuLi. – Leo Tolstoy, Anna Karenina

Kila mtu hufikiri kubadili dunia, lakini hakuna anayefikiri kujibadili mwenyewe- Leo Tolstoy

Usawa mwingi waweza kuwa wazimu. Na uwazimu ule mkubwa, kuona maisha kama yalivyo na sio yanavyohitaji kuwa- Miguel de  Cervantes Saavedra

Kuishi ni kitu cha nadra kikubwa dunia. Watu wengi huwa, hivyo tu. Oscar Wilde

Kila nayeishi kama kadri ya anayoweza huteseka kwa kukosa ubunifu. Oscar Wilde

Njia moja ya kupata mazao kutoka kwa maisha ni kuona maisha kama tukio- William Feather

Kitu cha muhimu ni kufurahia maisha yako- kuwa mwenye furaha- hayo ndio mambo yanayohitajika. Audrey Hepburn

Fanya hima kuishi au fanya hima kufa – Stephen King

Maisha yanaweza kueleweka kinyumenyume; lakini lazima kuishi kuenda mbele. – Søren Kierkegaard

Manufaa maishani ni kuwa wewe mwenyewe. Joseph Campell

Nimetambua kwamba ukipenda maisha, maisha yatakupenda kwa usawia. –Arthur Rubinstein

Maisha ni aslimia kumi kinachokutokea na aslimia tisaini vile wewe unavyoichukulia. Lou Holtz

Kama wapenda maisha, usipoteze wakati, kwa sababu maisha yameundwa na wakati. Bruce Lee

Hakuna mwanamume ambaye ameshindwa amabaye anafurahia maisha.- Wiiliam Feather

Maisha ya mtu ya ukweli ni tunapokuwa tukiota kama tuko macho. Henry David Thoreau

Maisha yangekuwa ya kutatanisha kama hatungekuwa wenye ucheshi. –Stephen Hawking

Hatufanyi matendo ya haki kwasababu tuna wema ama ubora, lakini afadhali tuwe nazo kwa sababu tumefanya matendo kwa haki. Sisi huwa kile tunachokirudia kufanya. Ubora basi sio tendo lakini tabia. Aristole

Kuna njia mbili pekee za kuishi maisha yako. Moja ni kama hakuna kitu cha miujiza. Ingine ni kama kila kitu ni miujiza. Albert Einstein

Sisi wote wajinga, lakini sio wajinga wa kitu kimoja. Albert Einstein

Kitu kubwa kwa kutoeleweka kwa dunia ni kueleweka kwake. Albert Einstein

Kuna nguvu kuu ya kuendesha kuliko mvuke, stima na nishati ya atomiki. Ni mapenzi. Albert Einstein

Jifunze kanuni za mchezo; Kisha cheza vyema kuliko wengine wowote. Albert Einstein

Niambie na nisahau. Nifunze na nikumbuke. Nihusishe na nijifunze. –Benjamin Franklin

Atakaye kuwa na subra atapata matakwa yake. Benjamin Franklin

Ni sawa kushangilia mafanikio lakini ni muhimu zaidi kuzingatia mafunzo ya kushindwa. Bill Gates

Mafanikio ni mwalimu mbaya. Hubemba hata waliowasomi kufikiri hawawzi kushindwa. Bill Gates

Kila mwanamme ana haki ya kuamua hatma yake mwenyewe. Bob Marley.

Hakuna mwingine ila sisi wenyewe tunaweza weka huru akili zetu. Bob Marley

Ukifanya kukaa na kubishana kila siku, unatoa maombi kwa shetani. Bob Marley

Afya ni zawadi kubwa zaidi, kuridhika ndio afya njema, kuaminika ndio uhusiano mwema. Buddha

Mjinga hujifikiri kuwa mwenye hekima, lakini mwenye hekima hujijua kuwa mjinga. Buddha

Usiishi kwa yaliyopita, usiote ndoto za wakati ujao, weka akili yako kwa mambo ya sasa. Buddha

Hakuna anayeweza kupa mawaitha ya hekima kama wewe mwenyewe. Marcus Tullius Cicero

Mtu mwenye ujasiri pia amejaa uaminifu. Marcus Tullius Cicero

Maisha ya wafu huwekwa kwa kumbukumbu ya wanaoishi. Marcus Tullius Cicero

Kutafuta, hata kwa mambo yale mazuri kabisa, lazima uwe na utulivu na ungwana. – Marcus Tullius

Mtu yeyote anaweza fanya makossa, lakini mjinga huendelea kwa makosa yake. Marcus Tulluis

Shukurani sio tu lile wema kubwa, lakini asili ya hayo yote mengine. – Marcus Tullius Cicero

Haijalishi uendavyo polepole mradi usisisimame. - Confucius

Maisha ni rahisi, lakini sisi husisitiza kuifanya magumu. - Confucius

Ushindi wetu mkubwa sio kwa kukosa kuanguka, lakini kusimama kila wakati tukiaanguka. - Conficius

Kila kitu kina urembo, lakini sio kila mtu huona. - Conficius

Popote pale uendapo, enenda na moyo wako wote. - Conficius

Chagua kazi upendayo, nawe hutapata kufanya kazi hata siku moja maishani mwako. - Confucius

Kwa siku mpya huja nguvu mpya na mawazo mapya . – Eleanor Roosevelt

Hakuna mtu anaweza kufanya kujihisi duni bila idhini yako. – Eleanor Roosevelt

Siku za usoni ni ya wale wanaoamini urembo wa ndoto zao - Eleanor Roosevelt

Hutasumbuka na watu wanavyokufikiria unapogundua vile kwa nadra wanavyofanya. - Eleanor Roosevelt

Fanya kitu kimoja kila siku kinachokuogopesha. – Eleanor Roosevelt

Kwa kila dakika umekasirika unapoteza sekunde sitini za furaha. - Ralph Waldo

Usiende ambapo njia inaelekeza, lakini enenda ambapo hakuna njia na uwache nyayo. - Ralph Waldo Emerson

Kukuwa mwenyewe kwa dunia inayojaribu kila mara kukufanya uwe kitu kingine ndio fanikio kubwa. - Ralph Waldo Emerson

Kila wakati fanya kile unachokiogopa - Ralph Waldo Emerson

Wakati wa giza tororo, unaweza ona nyota. - Ralph Waldo Emerson

Kile ufanyacho hunena kwa sauti ambapo siwezi sikia unachosema. – Ralph Waldo

Matumaini ni mazuri kwa kiamsha kinywa, lakini ni chakula cha jioni kibaya – Francis Bacon

Staajabu ni mbegu ya maarifa - Francis Bacon

Bila mziki, maisha yangekuwa kosa. – Friedrich Nietzsche

Kisicho kuua chakufanya mwenye nguvu. – Friedrich Nietzsche

Hakuna ukweli, maelezo tu. Friedrich Neitzsche