January 9, 2018

Muziki unaoongeza ubunifu katika kazi - Utafiti.

Nafahamu watu wengi tunapenda Muziki kusikiliza na wengine kusikiliza na kucheza sasa nikusogezee Utafiti uliofanywa Australia ambao umeonesha kuwa kusikiliza muziki uliochangamka sio tu kunaweza kuboresha hisia ya moyo, bali pia kunaweza kuinua uwezo wa kubuni.

Watafiti wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Sydney wametoa ripoti ikisema, katika utafiti wao mpya wamechagua miziki minne, ambayo inaweza kuleta hisia ya utulivu, furaha, huzuni na wasiwasi kwa binadamu.

Watafiti wamewagawanya washiriki 155 kwenye vikundi vitano na kuwataka kumaliza kazi zinazohitaji ubunifu, kama vile kufikiria matumizi tofauti ya ubunifu ya kupanga vitofali. Vikundi vinne vinasikiliza muziki wa aina nne unaoleta hisia tofauti, na kikundi cha tano hakisikilizi muziki.

Matokeo yameonesha kuwa, kusikiliza muziki uliochangamka kunaweza kuinua wazo la ubunifu. Watafiti wamesema, kuinua uwezo wa uvumbuzi ni jambo muhimu la kuhimiza maendeleo ya Sayansi na Teknolojia na ni muhimu sana kuelewa athari zinazotokana na muziki kwenye ubunifu. Mazingira yanaweza kuathiri ubunifu, na muziki ni moja ya njia zinazoweza kubadilisha mazingira.