January 27, 2018

Tamaduni 7 za Ndoa zitakazo kushangaza, huruhusiwi kutabasamu

Wanasema tembea uone au subiria usimuliwe….. kuna sheria au tamaduni ambazo zinatumika kwenye nchi mbalimbali na ukiziangalia unakuta ni tofauti na ulivyozoea au hujawahi kabisa kudhani kama kuna tamaduni hizo duniani.

1: Congo: Hauruhusiwi kutabasamu siku ya ndoa
Ni jambo la kushangaza na kuajabisha lakini ni katika kutimiza mila na desturi, unaambiwa Bibi na Bwana harusi nchini Congo wanatakiwa kuiweka furaha yao kwenye mashavu, hawatakiwi kutabasamu siku nzima ya harusi na kama watafanya hivyo itachukuliwa kuwa hawakuwa serious kuhusu ndoa.

2: Ufaransa: Champagne kwenye bakuli la chooni
Wanandoa nchini Ufaransa kulingana na tamaduni za baadhi ya sehemu hutakiwa kula chocolate na kunywa champagne baada ya mapokezi, hilo sio tatizo, ishu ni hii kuwa wanatakiwa kutumia bakuli la chooni kunywea champagne ambapo lengo la utamaduni huu ni kuwapa uimara na uvumilivu katika ndoa yao.

3: Urusi: Anayekata kipande kikubwa cha keki ndiye kiongozi wa familia
Wanandoa wapya Urusi wanatakiwa kuchangia mkate wa asili unaoitwa karavaya ambapo yeyote kati yao atakayekata sehemu kubwa ama mume au mke bila kutumia mikono ndiye atakuwa kiongozi wa familia.

4: Pakistan: Bwana Harusi kuibiwa viatu
Dada wa bibi harusi na ndugu wengine wa kike wanaruhusiwa kuiba viatu vya Bwana harusi na kama anavitaka lazima avikomboe kwa pesa ili virudishwe vikiwa salama.

5: Fiji: Jino la Papa kwa baba mkwe
Utamaduni wa ndoa katika nchi ya Fiji ni kuwa pale Bwana harusi anapoomba ruhusa kwa baba Mkwe ili ashikane na Mwanamke wakati wa ndoa lazima ampe baba mkwe huyo jino la papa.

6: Mauritius: Bibi harusi lazima awe na uzito mkubwa
Katika ndoa za sehemu nyingi duniani, Mabibi harusi hufanya diet kurekebisha miili yao na kupunguza uzito kabla ya ndoa lakini sio hivyo kwa Mauritius, Wasichana wadogo wanalazimishwa kula ili waongezeke uzito wakati wa ndoa zao ambapo hii ni kwa sababu wanaamini kuwa Mwanaume lazima awe na uwezo wa kumlisha.

7: Jamaica: Bibi harusi hupita mtaani
Hii inapatikana katika vijiji vya Jamaica ambapo wanakijiji hujipanga mstari barabarani kumuangalia Bibi harusi kwa lengo la kutoa maoni kuhusu muonekano wake ambapo kama watu wengi wataupinga, atalazimika kurudi nyumbani kubadilisha kisha arudi tena hadi pale wayakaposema anapendeza.