January 22, 2018

Mambo Kumi kupunguza ulaji mafuta kwenye gari lako

Mambo Kumi kupunguza ulaji mafuta kwenye gari lako

1. Peda yako yaani Ekseleleta isukume kwa utaratibu.

Hususani unapoanza mwendo; wengi hukosea kwa kuanzisha mwendo kwa ghafla na napendekeza kasi ya 50kph, na katika gia ya juu hivyo kama wewe ni mstaarabu katika uendeshaji wako nakuahidi hutakuwa na safari nyingi kwenda petro station.

Kama unakimbia uwe na sababu ya msingi kufanya hivyo jiulize unaenda wapi na je kuna haja ya kukimbiakimbia bila sababu ya kuwahi?, na kama unapaswa kukimbia basi fanya hivyo kwa uangalifu huku ukivuta mafuta kwa utaratibu.

2. Punguza mwendo kwa kuachia mafuta badala ya breki

Hapa namaanisha kama unataka kupunguza mwendo hata kama ulikuwa katika mwendo wa juu jifunze/jizoeze kuachia mafuta badala ya kutumia breki hii itakusaidia kwa kuokoa mafuta ambayo yangetumika bila sababu, mathalani katika foleni inayoenda taratibu huna haja ya kutumia zaidi peda ya mafuta badala yake achia breki wakati gari likisogea taratibu.

3. Usisukume Peda ya mafuta hadi chini 

Kupeleka peda chini tena kwa haraka hakumaanishi utapata matokeo ya mwendo wa juu badala yake utatumia mafuta mengi bila sababu, hata kama unasafiri masafa, balance gia unayotumia na namna unavyovuta mafuta.

4. Je ni lazima utumie kiyoyozi?

Kuna kasumba hususani miji au maeneo yenye joto madereva kutumia kiyoyozi kila wakati bila kujali ni majira gani,iwe wakati wa joto,baridi,unyevu nk yeye na kiyoyozi tu...Aah ndugu yangu unameza mafuta bila sababu, be conscious na pesa zako (hata kama zipo tele) nidhamu ya matumizi ni utamaduni mzuri, hata kama husave kwa ajili yako save for the needy au kwa ajili ya mazingira.

Kama eneo ulilopo halina vumbi na hali ya hewa si ya joto sana inapobidi shusha vioo vya gari lako tumia hewa asili , kula upepo kwa raha zako, aircon wakati wote pia inaweza kuwa si salama kwa afya yako, mind you ile ni artificial air.

5. Je, upepo wa matairi umejaa kiasi kinachopendekezwa?

Tafadhali zingatia kwamba upepo mdogo kwenye matairi yako sawasawa na matumizi makubwa ya mafuta,napendekeza chunguza upepo wa matairi yako kila baada ya wiki mbili kabla ya kuondoka na gari lako asubuhi, usipime upepo wa tairi baada ya kutembea au wakati gurudumu lina joto. Na ili kujua upepo unaohitajika kwenye matairi ya gari lako angalia kwenye mwimo wa mlango wa dereva pale waundaji wa gari huweka vipimo vya upepo vinavyofaa kwa gari lako, au kama hilo ni gumu endesha hadi jirani na gereji au sheli iliyopo jirani nawe wakuchekie matairi.

Usiweke matairi yasiyo asili kwa gari hilo,mathalani unaweka matairi makubwa kuzidi muundo wa gari hilo pia linasababisha mafuta kwenda mengi.

6. Usibebe uzito usio na lazima kwenye gari lako.

Kila mzigo ndani ya gari lako uwe na sababu ya kuwemo humo na wenye manufaa kwako ama vinginevyo.

Gari lako linahitaji mafuta mengi zaidi likiwa na uzito mkubwa. Ni kama wewe ukibeba mzigo mzito unavo sweat ndo hivo hivo kwa gari, kwa hiyo chunga! Kwa kadiri uzito unavyokuwa juu ndivyo mafuta mengi zaidi yanavyoenda. Kooh! wale waomba lifti wa kila siku wawe wanachangia mafuta kkk.

7. Epuka foleni

Mtu ataniuliza kwa vipi.
Amka mapema au tumia njia mbadala au ondoka muda ambao foleni sio kubwa sana nk nk.
Kumbuka kwa kadiri foleni inavyokuwa ndefu na haitembei kwa haraka ndivyo mafuta yanavyotumika zaidi. Hii ni kutokana na ile simama,tembea,simama,tembea kwa sababu muda huo kila unapoanza iwe ni kwa gari la manual au aotomatic gia ya kwanza ndiyo huanzisha mwendo na gia hii humeza mafuta mengi tofauti na gia za juu...Lakini kumbuka unapokuwa katika foleni kulegeza gia liva yako katika free isiwe engaged hii husaidia kupunguza ulaji wa mafuta, usizime na kuwasha gari ukiwa foleni hiyo haisaidii na inameza mafuta zaidi kuliko silence.

8. Lifanyie gari lako matengenezo (service) kila inapobidi

Ubora wa Oili ya gari lako unaathiri kwa namna moja ama nyingine ulaji wa mafuta kwenye gari lako, wakati wote zingatia kuwa ni muhimu kufanya matengenezo ya gari lako huku ukitumia vifaa halisi kama vile oili halisi,filta halisi nk nk Badilisha oili kwa wakati kama inavyopendekezwa na muundaji wa gari lako

9. Ondoa Keria kwenye gari lako

Haya magari tunayonunua nchi za wazungu na waasia huwa mengine yanakuja na keria ambazo wenzetu huko walikuwa wanazitumia kwa matumizi fulani labda kubebea mizigo au wanyama lakini sie huku afrika ni nadra kwa gari binafsi kubeba mizigomizigo...sasa keria hususani kwenye magari madogo linakawaida ya kuongeza ukinzani wakati unaendesha hivyo kwa asilimia fulani kupunguza ufanisi wa mwendo na kuongeza ulaji wa mafuta. Funga keria wakati unapoihitaji tu.

10. Unapokuwa barabara kuu na katika mwendokasi wa juu funga madirisha au dirisha la juu

Unapoikimbiza gari kwa mwendo kasi wa zaidi ya 80kph hususani kwa umbali mrefu bila kupunguza mwendo...muundo wa gari lako unamata sana,,,kwanini kwa sababu watengenezaji wa gari hilo waliliunda kwa namna ambayo litaweza kukabiliana na upepo hivyo kurahisisha uendaji wake, sasa ukiweka madirisha wazi wakati wa mwendo mkubwa unaruhusu hewa ndani ya gari na matokeo yake ni kuathiri mwendokasi wa gari lako na hatimae kuathiri namna gari linavyotumia mafuta.

Waundaji wa magari huita aerodynamics na huamini kwamba hili ni muhimu katika kusaidia gari lako liende kiulainii kabisa na kama inabidi upate hewa basi tumia vitundu vya hewa inayoletwa kwenye gari lako na feni au washa AC,lakini AC unarudi kulekulee!

NYONGEZA: Usifanye safari zisizo za lazima wenyee mnaita misele huko ni kuchoma hela bila sababu.

Jifunze kubana matumizi kama una ndoto za kufanikiwa zaidi kiuuchumi, ila kama umeridhika na ulipo poa tu.