January 16, 2018

Madhara ya kutazama picha na video za ngono (porn).

Picha za ngono pamoja na video za ngono "Ponografia", Kwa kizazi hiki zimeenea kila kona katika televisheni, sinema, Simu, Computer, video za miziki na internet pia. Je! Picha na video izo za ngono hazina madhara kwetu, kama wengi tunavyo dhani?

Leo tutatazama madhara ya picha na video za ngono kwa vijana, katika makala nyingine tutatazama adhari za picha izo kwa watu wazima, kisha adhari za picha na video ngono kwenye mahusiano.

Madhara ya kutazama picha ba video za ngono kwa Vijana. 
Takwimu zinaonyesha kwamba watazamaji wengi wa video na picha za ngono (ponografia) ni vijana tena chipukizi, hasa wavulana wenye umri wa miaka kati ya 12-17. Asilimia kubwa ya vijana hao hujifunza na kujiingiza katika  maswala ya ngono, wakiwa katika umri mdogo huku chanzo kikiwa na picha na video za ngono wanazotazama.

Baada ya vijana hao kujifunza na kuingia katika maswala ya ngono kitu kinachofuata ni ongezeko la mimba zisizo rasmi kwa hawa vijana wadogo na kuongeza kasi ya magonjwa ya zinaa kama vile UKIMWI n.k. huku chazo kikiwa ni picha na video hizo za ngono ambazo watoto wetu wanazo kwenye simu na laptop zao.

Uchunguzi wa athari za sauti na picha za uchi (Ponografia) katika utendaji wa kawaida wa ubongo unaonyesha kwamba kutazama picha hizo huathiri kabisa uwezo wa kawaida wa kufikiri. Pia hudhuru ubongo wa watoto unaoathiriwa kwa urahisi kwa sababu hufanya wasione mambo kihalisi na hudhuru afya yao ya kiakili na ya kimwili, na huwazuia kupata furaha.Alisema Dakt. Judith Reisman, mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Vyombo vya Habari.


Tazama video: Majaribu ofisi ya Mchungaji, nyie wadada Mungu anawaona!