January 17, 2018

Vijana 50 wa kitanzania wenye ushawishi zaidi.

Tuzo za Vijana 50 wa Kitanzania wenye Ushawishi (50 Tanzania Most Infuential Young Tanzanians) zilizoandaliwa na Avance Media zimetangaza washindi wake jana January 16, 2018.

Mwanasoka Mbwana Samatta ameshinda kwenye category ya Michezo, wakati wakili Peter Kibatala yeye ameshinda kwenye category ya Sheria na Uongozi, Yusuph Bakhresa akichukua tuzo kwenye category ya Biashara.

Wengine ni Mwanamuziki Alikiba ambaye amechukua tuzo ya Burudani, Faraja Nyalandu akichukua category ya Biashara za Kijamii na Asasi za Kiraia, Mitindo ya Maisha tuzo yake imechukuliwa na Jackline N. Mengi na tuzo ya Sayansi na Teknolojia imechukuliwa na Jumanne Mtambalike.

Mbwana Samatta pia amekuwa Mshindi wa Jumla (Overall Winner) kwa kupata kura nyingi zaidi kuzidi wote walioshindania tuzo hizo akifuatiwa na Wakili Kibatala na Millard Ayo.