January 8, 2018

Wanandoa wauza mali zao zote ili wasafiri dunia yote.

January 8, 2018 nimeipata stori ambayo inaweza ikakushangaza ni kutoka Uingereza ambapo wanandoa Faye na Matthew Gooding na watoto wao watano wameamua kuuza nyumba yao na vitu vyote wanavyomiliki ili kusafiri duniani kote.

Wawili hawa wakiwa na watoto wao Ralph, 9, Judah, 7, Hunter, 4, na mapacha Freddie na Jasper, wenye miezi 10 wameuza na kugawa mali zao wakati wa kipindi cha sikukuu za Krismas na kueleza kuwa japokuwa sio rahisi kuachana na mali zao walizozichuma kwa miaka mingi bado inawapa uhuru kufanya kile wanachokipenda.

Mr Gooding ameeleza kuwa safari yao ya kuzungukia dunia itaanzia Sweden ambapo wana marafiki wengi wanaoishi huko na kwamba watoto wao Ralph na Judah ndio watapendekeza baada ya Sweeden waende wapi.

“Tunategemea kuiona Ulaya kwa miaka miwili, baadaye Japan, Marekani, Bali na Thailand, watoto wetu hawatakwenda shule lakini mimi na mke wangu Faye tunaamini watajifunza mengi zaidi kupitia safari hii.”Mr. Gooding