January 11, 2018

Zawadi bora ya kumpatia mwanamke ni ipi? majibu yako hapa

Kununua zawadi ambayo itampendaza mtu wa jinsia tofauti na yako ni kazi ngumu sana. Kwa sababu mtazamo wa wanaume na wanawake ni tofauti kabisa.

Inachanganya sana na inaweza kuleta matatizo pale tunapotakiwa kununua zawadi kwa ajili ya jinsia tofauti, kwa sababu mara nyingi tunajikuta tukinunua zawadi ambayo "tunadhani" ataipenda na siyo ile anayoipenda. 

Ikiwa unatafuta zawadi kwa ajili ya mwanamke, awe mama yako, mchumba wako ama shangazi yako, ni muhimu sana kuelewa ni nini wanawake wanatafuta katika zawadi yako kwanza!

Wanawake wanathamini sana upendo na kuwajali kuliko zawadi yenyewe. Wanawake huwa na tabia ya kutaka kujua (ndani yao) kwa nini unampatia zawadi hiyo. Kwa hivyo mawazo yako na hali ya kujali unayoiweka katika hiyo zawadi ni muhimu zaidi kwa wanawake kuliko zawadi yenyewe. 

"Tunapenda sapraizi, na tunapenda kujua kwamba unajali pia. Kwetu wanawake, kujali kwako na mawazo yako juu yetu yana sauti kubwa sana" - Anna Chui.

Wanawake wanapenda sana zawadi, tena hupendelea zaidi "Practical gifts", wanapenda kupokea zawadi za pekee ambazo hawawezi kujinunulia wenyewe. Wanawake hujitahidi sana kununua vitu kwa ajili yao, lakini pamoja na kununua vitu vingi huwa hawajui ni kitu gani ambacho ni maalum sana kwao.