February 7, 2018

Dalili 6 kwamba unahitajika kusitisha uhusiano hata kama bado unampenda.

Maisha hayana kanuni maalum, waweza kujikuta unaingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu wa ajabu kabisa na pia yawezekana mtu uliyotamani kuwa naye akakubali kuwa nawe lakini mambo yakaenda tofauti na yalivyokuwa matarajio yako. Yawezekana ikaonekana jambo la ajabu kutafuta ishara za kuachana na mpenzi wako japo kuwa bado unampenda, lakini uhusiano wa kimapenzi unaweza kukatishwa kutokana na sababu nyingi zaidi ya mwenza wako kuwa na mchepuko, na hizi ni ishara sita za kuanza kufikiria kukatisha uhusiano huo kama utaona zinajitokeza mara kwa mara.

1. Unapokuwa huna furaha
Moyo unataka unachokitaka na unataka upewe unachokitaka. Mara nyingine yawezekana moyo wako hauna haja na mpenzi wako wa sasa ambaye ni mzuri, mkarimu na mcheshi. Mara nyingine unachohitaji moyo wako ni kuachana na mpenzi wako ambaye ni mvivu, mbinafsi na katili. Haijalishi sababu ni nini, lakini jambo moja ni la kuzingatia sana: huna haja ya kuendeleza uhusiano wa kimapenzi na mtu kwa sababu tu hutaki kumuumiza.

2. Kama unataka kitu kingine tofauti
Kuwa na watoto. Kubadili kazi. Kuhama mji. Kununua nyumba. Maamuzi kama haya ni makubwa ambayo inabidi mkubaliane kuyafanya. Wapenzi walio tayari kuacha au kufanya jambo kwa ajili ya mwenzie huwa ni uhusiano wenye furaha. Hata kama unampenda mtu kiasi gani, mara nyingine maisha yanawaelekeza kwenye njia tofauti. Kama kweli unaitaka kazi uliyopata mji au nchi nyingine na mpenzi wako hataki kabisa uondoke, si lazima ukubali kwa ajili yake. Baadhi wanafikia muafaka lakini wengine hawawezi. Ikiwa hivi, hii ni ishara kwamba uendelee na mipango yako.

3. Kama kila muda unawaza kuachana naye
Huna haja ya kuwa na sababu. Kama kila mara unapata mawazo na fikra za kusitisha uhusiano wako, hata kama huna hakika sababu hiyo ni ipi, muda wa kuendelea na maisha yako umefika. Yawezekana ukaumia kwa kumuacha lakini pia yawezekana ukahisi umetua mzigo mkubwa uliokuwa unakuelemea. Hisia zote hizo ni za kawaida. Usijione kuwa ni mkosaji sana.

4. Hamfikii suluhisho la migogoro yenu
Mara nyingine unafanya kila jitihada kuwa katika uhusiano mzuri lakini mnajikuta mnagombana kwa mambo yaleyale. Au mna mgogoro mkubwa na kwamba kila mnavyojaribu hamfikii muafaka wa kuitatua na kusababisha kila zuri kwenye uhusiano wenu lisahaulike. Huwezi kumlazimisha mpenzi wako abadilike. Kama hamuwezi kupata muafaka wa tatizo lenu, au kama ni jambo linalohitaji mabadiliko makubwa ambayo hutaki kuyafanya basi yawezekana ni wakati muafaka wa kuanchana kabla mambo hayajaharibika zaidi.

5. Hupati unachohitaji
Watu wengine hawawezi mapenzi ya mbali. Wanahitaji kuwa karibu na wapenzi wao. Baadhi wanapenda kuwa na mpenzi mkimya, mwenye kujali na baadaye wanagundua kuwa hawawezi kuendelea na uhusiano na mtu wa aina hiyo. Wengine wanajikuta kwenye uhusiano na mtu ambaye anahitaji mambo tofauti kabisa na anayohitaji yeye.
Yawezekana mtu wa aina hii ndiye uliyekuwa unamhitaji lakini mwisho wa siku, kama mahitaji yako hayatimii yawezekana ufikiria kukatisha uhusiano huo. Ni sawa kujiweka mbele kwenye vipaumbele vya maisha yako.

6. Kama anakutesa
Hili ni jambo ambalo watu wengi walio kwenye uhusiano hawapendi kulizungumzia, lakini ni kawaida kabisa kujisikia vibaya baada ya kuachana na mtu ambaye alikuwa anakunyanyasa kiakili, kimwili au kimapenzi. Hilo halimaanishi kuwa unatakiwa kumng’ang’ania, inamaanisha unatakiwa kufikiria mambo mengine na kuendelea na masiha yako.
Kuachana na mpenzi ni jambo gumu, lakini ni gumu zaidi iwapo mtu unayeachana naye bado unampenda na kumjali. Kama umeshafikia uamuzi wa kuachana na mpenzi wako, jiamini mwenyewe na maamuzi yako, mara zote.