February 2, 2018

Download app ya azam tv live.

App ya Azam TV live. App ya kisasa kabisa ya AzamTV imeanza kupatikana rasmi katika Google Play Store na App Store ya Apple kuanzia Julai Mosi.


App hiyo iliyokuwa ipatikane tangu Juni mosi lakini ilishindikana, watu wataweza kutazama chaneli saba ambazo ni Azam ONE, Azam TWO, Sinema Zetu, ZBC 2, Azam Sports HD kwa Tanzania Pekee, na Real Madrid TV na NTV Uganda.

App ya Azam TV live
Taarifa moto moto za Kimichezo, Habari, Burudani na matukio mbalimbali yanayoendelea nchini na ulimwenguni pia yatapatikana kupitia App hiyo.
Kwa sasa Kuangalia chaneli hizo hakutatozwa pesa yoyote yaani ni bure ingawa mwanzoni ilitaarifiwa kulipia kwa Tsh 400 kwa siku, Tsh 2500 kwa wiki au Tsh 9000 kwa mwezi.

Isikupite hii: Sababu za wanawake kulia baada ya kufanya mapenzi

App ya Azam TV live
Ili kuweza kufurahia huduma zao, hakikisha una bundle la kutosha tu na network nzuri ili uweze kufaidi vizuri huduma zao mahali ulipo na wakati wowote.
3G ndio mtandao wa chini kabisa unaotakiwa kuutumia kupata huduma hii kwenye AzamTV app.
Kituo kingine cha Runinga ambacho kilishatangaza App yao ni ITV ambayo inapatikana Google Play Store na App Store ya Apple