February 16, 2018

Faida nyingi za kiafya za kutumia uyoga.

Uyoga ni miongoni mwa vyakula adimu sana duniani. Lakini ni miongoni mwa vyakula vyanye virutubisho muhimu sana kiafya tofauti na watu wengi wanavyodani.

Kwa mujibu wa mtandao wa www.organicfacts.net uyoga una vitamini na aina nyingi za madini.Baadhi ya virutubisho vilivyothibitishwa kuwemo kwenye uyoga ni pamoja na Vitamini B2, B3, B5, B6, B Complex pamoja na madini ya Potasiamu na ‘Phosphorus’.

Wataalamu hao wanaeleza kuwa virutubishoi vilivyomo ndani ya uyoga kuwa vina uwezo mkubwa sio tu wa kuimarisha kinga mwilini bali pia kupambana na maradhi.

Mtandao huo pia umeendelea kueleza kuwa uyoga ni chanzo kingine kizuri cha madini ya chuma na shaba yanayohusika katika uwezeshaji wa usambaza wa hewa ya oksijeni mwilini.

Vitamini B2 inayopatikana kwenye uyoga, ni tiba kwa watu wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kichwa unaojulikana kama ‘kipanda uso’.

Kwa kula kiasi kidogo cha mmea huo utajiweka kwenye nafasi ya kuwa na hali nzuri hususani kwa wale wagonjwa wa kipanda uso

Vitamini B kwenye uyoga, ina uwezo wa kuzuia uchovu wa mwili na akili hasa wakati wa kazi nyingi. Vitamin B3 husaidia kupunguza kiwango cha lehemu mwilini, wakati Vitamini B6 huondoa hatari ya mtu kupatwa na kiharusi au shambulio la moyo.

Pia, una madini ya zinki yanayoimarisha kinga ya mwili pia husaidia kuponya haraka vidonda si hivyo tu faida nyingine husaidia ukuaji mzuri wa seli za mwili, huimarisha kiwango cha sukari mwilini na kukufanya usikie ladha , harufu ya vyakula na vitu vingine ipasavyo.