February 16, 2018

Hii ndio top 5 ya fashion za viatu vya wanawake (michuchumio)

1. Christian Louboutin
Christian louboutin wamekua juu kwa mwaka huu na kuonesha ubunifu mkubwa katika kutengeneza viatu vya kike vyenye ubora na urembo ambao umefanya hata baadhi ya mastaa kuvivaa kwenye Red Carpet Events mbali mbali.


2. JIMMY CHOO
Kutoka kwa designer wa Malaysia Choo Yean, viatu vya jimmy choo vimepata umaarufu sana barani Europa vikiwa na mitindo mbali mbali ambayo huweza kuvaliwa ofisini, kwenye sherehe mbali mbali na hata viatu vya michezo.


3. PRADA
Prada ni kampuni ya muda mrefu sana katika ubunifu wa viatu vya wanawake na mpaka sasa inashikilia nafasi ya tatu katika mstari wa viatu vya ubunifu vya wanawake. Prada zinasifika sana kutokana na hali yake ya kupenda kua na upekee kimuundo ambapo kila toleo jipya hua tofauti na toleo la awali yake.


4. MANOLO BLAHNIK
Kutoka Hispania, manolo ni moja wapo kati ya viatu vya kike vilivyopewa midani ya juu katika ubunifu mwaka 2013. Manolo ameweza kukamata zaidi soka la Ulaya pamoja na Amerika kusini akiwa na mitindo mingi zaidi kwa viatu vya harusi na pia kikazi.


5. GUCCI
Kutokea mwanzo wa karne ya 19, gucci imejikita kwenye kilele katika maswala ya mavazi kwa wanawake, wanaume na hata watoto. Kwa upande wa wanawake, Gucci imeweza kuleta bidhaa nyingi ambazo zimekua zikivaliwa na watu wa aina mbali mbali huku ikipewa promo kubwa na wasanii mbali mbali.