February 23, 2018

Historia fupi ya maisha ya mpendwa wetu Akwilina Akwilini. (Tutakukumbuka daima)

Akwilina alizaliwa tarehe 1 Aprili, 1996, katika Kijiji cha Marangu Kitowo, Kata ya Olele, wilayani Rombo, Kilimanjaro.

Alipata elimu yake ya msingi katika Shule Kitongoria na kuhitimu 2009. Halafu baadaye sekondari alisomea mkoani Iringa na kuhitimu 2014. Baadaye, alichaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Embauwai, iliyoko Ngorongoro, Arusha.

Kutokana na afya yake kumletea shida akiwa mkoani Arusha, ililazimika kuhama mkoa na kwenda kumalizia elimu ya sekondari kidato cha tano na sita tena mkoani Iringa na kumaliza mwaka 2016.

Kuanzia Oktoba 2017, alianza masomo yake katika chuo kikuu cha usafirishaji (NIT) hadi umauti unamfika 16 Februaria, 2018. Hapo NIT alikuwa anachukua shahada ya kwanza ugavi na ununuzi.

Tukio hili la kusikitisha limeamsha hisia kali sana katika mitandao ya kijamii nchini Tanzania. Wengi wamelaani kitendo cha askari kutumia risasi za moto kutuliza ghasia za kisiasa. Tena kwa watu ambao hawana silaha yoyote na wanafanya maandamano ya amani bila fujo.