February 3, 2018

Idris Sultan ataja aina ya wanawake anaowaogopa na kuwaheshimu.

Msanii maarufu wa filamu Tanzania na mchekeshaji Idris Sultan amefunguka na kusema kutaja wanawake anaowaogopa duniani.

Idris alipokuwa katika mahojiano na kiindi cha Kikaangoni Live kinachorushwa na runinga ya EATV, alisema kuwa, katika wanawake anaowaogopa duniani ni pamoja na wanawake wa marafiki zake na wanawake wa watu, na kukiri kuwa hawezi kutoka nao hata siku moja.

“Siku hizi naogopa sana wake za watu, maana ukishaona mtu wako wa karibu kanyolewa kipara basi ujue kinachofuata ni kitu kibaya sio kizuri. Sijawahi kutoka na mke wa mtu na sijui kama hata ilishawahi kutokea kwa bahati mbaya, ila hata mimi sitataka kusikia kuwa kuna mtu katoka na mke wangu alafu kusiwe na msiba kwangu au kwao. Lazima kuwe na namna ya kuadabishana kwa mambo madogo madogo kama hayo. Yaani umetoka na mke wa mtu na mimi natoka na maisha yako. Kwahiyo mimi sitaki kugusa mke wa mtu kwa sababu hata mimi sitaki kugusiwa wa kwangu,” alisema Idris.

Aliongeza kuwa hapendi pia kutoka na wanawake ambao ni ndugu wa marafiki zake na huwa anajiweka mbali naoi li kuepusha mizozo inayoweza kuibuka kati yake na Rafiki zake pindi watakapogundua kuwa ana mahusiano na nugu zao.

“Girlfriend ni kitu cha kupita tu ni kama kikombe na sahani, kila mtu anaweza kukitumia au kukiacha au labda awe amefanya commitment fulani na kumchukua kuwa mke. Hapo tunakuwa tunaongea lugha nyingine tena, ila katika vitu vingine pia ninaogopa ni ma-girlfriend wa maraki zangu au watu wao wa karibu, hao nawaogopa sana,” alisema.

Idris alishawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mrembo aliyekuwa Miss Tanzania, Wema Sepetu lakini mahusiano hayo hayakudumu kwa muda mrefu kutokana na drama nyingi zilizokuwepo katika mahusiano hayo, lakini pia Idris alikiri kuwa Wema anaweza kuwa ndiye mwanamke pekee aliekuwa nae katika mahusiano na akawa anajisikia vizuri sana na ni mwanamke ambaye hatoweza kumsahau katika maisha yake pia, kwa sababu aliweza kumbebea mimba ingawa mimba hiyo iliharibika.