February 8, 2018

Jinsi ya kurekebisha mzunguko wa hedhi. Soma hapa

Kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi huanza ghafla au polepole ambapo mwanzo mwanamke alikuwa akipata siku zake katika utaratibu unaoeleweka lakini mara haelewi au hajielewi namna mzunguko wake unavyoenda.

Kufuati hali hiyo wanawake wengi hupata hofu juu ya mzunguko na huamua kutumia dawa ilikuurudisha katika mfumo wake.

Madhara yanayoweza kutokwa endapo kukawa na mvurugiko ni pamoja na:- kushindwa kupata ujauzito, maambukizi katika kizazi na kuziba kwa mirija ya uzazi.
Vitu vinavyosababisha kvurugikwa kwa mzunguko ni pamoja na kuwa na Msongo wa mawazo, Uvimbe kwenye kizazi, woga, hofu , Kutokwa na uchafu ukeni na Matatizo kwenye mfumo wa homoni.

Jinsi ya kurekebisha mzunguko wa hedhi:-
a.)Papai
Pendela kula matunda ya papai kwani carotene, chuma ( iron), Kalsiamu (calcium) na vitamini A na C ambavyo husaidia kulainisha na kunywea kirahisi kwa kuta za mji wa uzazi.

b.)Kunywa maji
Takribani magonwa mengi chanzo chake ni mwili kutokuwa na maji ya kutosha. Maji ni uhai. Unachohitaji hapa ni kutokusubiri kiu.

c.)Tangawizi
Utumika kama kiungo cha chai ama kcha kwenye chakula, lakini tangawizi ni moja ya kiungo kinachotimu maradhi mengi sana.
Tangawizi hufanya kazi mhimu kabisa katika kushusha kiwango cha homoni inayosababisha maumivu ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘prostaglandins’.