February 7, 2018

Mambo 5 wanawake wanatamani uyajue wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Kuna baadhi ya vitu ambavyo wanawake hutamani sana wanaume zao wawe wanajua katika mambo mengi, ili wasipate shida ya kumwambia mara kwa mara, jambo ambalo si wanawake wengi huwa na guts za kumwambia mtu, hapo ndipo unakuta mara nyingi mwanamke anaanza kuchepuka na kwenda kwa mtu mwingine wa kawaida tu kupata mahitaji yake. Basi usikonde, haya ni baadhi tu ya mambo ambayo wanawake wengi hutamani wanaume wawe wanajua kabisa bila hata ya kuambiwa.

1. Ujasiri si sawa na kutumia nguvu

Kuna wanaume wengi huwa hawajui tofauti ya ujasiri na kutumia nguvu, hivyo wasikiapo kuwa inabidi uwe na ujasiri wanadhani kuwa kuna kutumia nguvu, wanawake wengi wamekuwa wakikerwa na kuogopeshwa na mambo ambayo hufanyiwa na wanaume zao, kipindi ambacho wanaume wakufikiri kufanya hivyo ni kuwa na ujasiri. wanawake hutamani sana wanaume wangejirekebisha na kujua maana halisi ya kuwa na ujasiri.

2. Sio wanawake wote hupenda vitu sawa

Hapa inatokea wanaume wengi kukariri kuwa, sababu tu ex-wake alikuwa anapenda kufanyiwa vitu fulani, basi na huyu wa sasa atakuwa hivyo hivyo, hii inatokea kuwachanganya sana wanawake, na kukereka kwa baadhi ya mambo, huku mwanamke akiwa hana jinsi bali kuvumilia tu, na mwisho wa siku ndio unakuta, ananza kutafuta way-out ya kukukwepa.

3. Hupendelea tendo la ndoa lidumu zaidi ya dakika mbili

Wanawake hupenda hata ikibidi ifanyike siku nzima, ila cha zaidi si muda ambao una-matter, imetokea wanaume wengi kujali kujizuia, ilimradi wa-last muda mrefu katika tendo, but kutokana na tafiti hili sio ishu kabisa, wanawake wengi hupenda zaidi ya muda mrefu, hupenda ku-establish connection wakati huo, ambao unafanyika through Kissing etc vitu ambavyo wanaume wengi huwa hawafanyi na kukazania tu kukaa muda mrefu kujua kuwa ndio wanawake wanachotaka.

4. Wanawake wanapenda ufuate anachokitaka

Iko wazi sana kuwa mara nyingi kujua kuwa mwanamke anahitaji nini, ni kitendawili kwa wanaume walio wengi, hivyo ni vizuri kuwa makini na kugndua ni kitu gani hapendi, hii hutokea cause mara nyingi si wanawake wote wanaweza kukwambia ni nini hasa kinawauzi, kuogopa kukuudhi, hivyo inawafanya wapate shida sana na kuweka maisha yao yawe magumu, ila hupenda sana kuwa makini na matendo yao ili kujua tofauti ya vitu ambavyo hawapendi na vile vinavyowapa furaha.

5. Ni zaidi ya mapenzi na sio ufundi

Ni kweli wanawake wengi hukubali kuwa kuna wanume wenye ufundi/uzoefu katika haya mambo, ila hiyo sio ishu zaidi, kinachotakiwa ni mapenzi, kuonyesha mapenzi na dalili zote za kumjali ndio jambo muhimu sana. Baadhi ya wanawake wamewahi kufunguka na kukiri kuwa tztizo la wanaume zao si kitandani, ila ni mapenzi kwa ujumla yanapungua.