February 7, 2018

Mambo 6 msichana usiyopaswa kufanya kama upo single.

Siku ya leo naomba nizungumze na wale wadada wote ambao hawajoelewa au kwa kibantu huitwa (single ladies). Ewe mwanadada yapo mambo ya msingi ambayo unapaswa kuyafahamu kabla ya kuolewa na mambo hayo ni;

1.Usiharakishe kutoka nyumbani kwa wazazi wako kwa gia ya kwenda kuolewa.

2.Usimsubiri mwanaume mpaka aje ndio uanze kuishi. Unaweza kuishi maisha timilifu hata ukiwa huna mwanaume.

3.Achana na pombe zimewauwa wenzako wengi kwa kisingizio cha kuondoa stress na wewe unaweza kufa pia.

4.Usiwe mtu wa kuendekeza kuzipokea na kuzijibu namba ngeni za simu hasa nyakati za usiku.. sio njia sahihi ya kupatia mpenzi.

5.Tengeneza mazingira ya kuilinda afya. Jitahidi Kunywa maji mengi na Chakula kwa diet achana na viofa ofa vya bure, vimesha waponza wenzio wengi mpaka sasa.

6.Vaa vizuri na kiheshima. Watu watavutiwa na wewe ulivyo kabla ya kuongea nawe