February 2, 2018

Sms nzuri za kusimumua kwa wapenzi (Wanandoa)

Ukipata tutakula na wala usijali mpenzi wangu.
Ukikosa tutalala na hiyo itabaki siri yanguuuuuuuu.nakupenda mpenzi
.....................

Raha ya ndege kichaka si tunduni asilani,
Raha ya Ndege ujumbe nakupa mpelekee
mwandani iwapo hukumkuta msubiri mlangoni,
Usije ukaondoka hakuchinji asilani,
Mwambie namkumbuka hatoki mwangu moyoni.
ucku mwema
     ..............................

Usiku wa leo uwe ni wenye faraja kwako, utawaliwe na usingizi wa mahaba kwenye kope zako, naomba ujenge taswira yangu katika mawazo yako, Usisahau kuniota sweet wangu. USIKU MWEMA

*°·.¸¸.° ? °·.¸¸.°*


Hata kama nitajidanganya kwamba sikupendi, moyo wangu umeganda kwako na hakuna dalili za kukuacha, wewe ni wangu peke yako dear...
................


Maji hunitosha nisikiapo kiu, chakula hinitosha nisikiapo njaa, lakini wewe hunifaa kwa kila kitu!
.............


Wewe ni mng’arao machoni mwangu;
Tabasamu la midomo yangu;
Furaha ya uso wangu;
Kwa sababu bila wewe, mimi sinajipya.
................


Moyo wangu kwako hautavunjika kamwe. Tabasamu langu kwako halitafutika kamwe. Penzi langu kwako halitaisha kamwe. Nakupenda!
................