February 6, 2018

Tabia 20 za msichana anayekupenda kimapenzi lakini hawezi kusema.

1. Atakutega kupata attention yako.
Hufanya mambo ambayo yatamfanya kuona kama unampenda au lah! Mf wa mambo hayo ni kujifanya anaumwa na kuangalia respond yako kwake ni kiasi gani unamjali na kiasi gani utahangaika kwa ajili yake au

2. Haoni aibu kugusa sehemu yako ya mwili.

Msichana anayependa haoni aibu kukushika mkono ama kukutomosa au hata kukumbatia. Kwa kufanya hivyo hujua kuwa kwa asilimia kubwa hisia za kushikana kwenu kutamrahisishia kazi ya kuwa na wewe

3. Kucheka kwa nguvu hata kwa kitu kisicho chekesha endapo wewe umezungumza.

Mara nyingi ataonesha uso wa furaha hata kama si furaha ya kweli

4. Wivu.

Hujisikia wivu anapokuona na wasichana wengine. Ukiwa unachart nao na ukiwaita majina ya kimahaba. Hapendi.

5 anakumbuka siku zako muhimu.

Hukumbuka kama vile siku yako ya kuzaliwa hatowez kuisahau kufanya ipite bila kukutakia heri ya siku ya kuzaliwa kama sivyo ukifaulu mtihani au chochote katika maisha yako atakuwa mbele kukupongeza

6. Eye contact anapenda kukuangalia machoni muda wote ambao mtakuwa mkizungumza pamoja akidhani kuwa utaelewa ni kiais gani anakupenda kupitia vile ambavyo anakuangalia. Ila wengine huona aibu kuwatazama wavulana wanaowapenda si wote wana ujasiri wa kuwatazama wapenzi wao.


7. Hupenda kukaa mmuda mwingi na wewe.

Hawezi kupoteza hata sekunde ukimuhitaji kwa mazungumzo. Anajisikia furaha kukaa na wewe muda mrefu bila kuchoka. Anaweza akaacha kila kitu anachokifanya ili ajumuike na wewe.

8. Yupo tayari kuangamiza.

Kama msichana anakupenda yupo tayari kusacrifice. Ni kitu ambacho hakuna mtu ambaye anaweza akafanya kwa mtu mwingine. Utaona vipi huyo msichana alivyo kwako na wa wengine. Yaani yupo tayari yeye akose lakini wewe upate na kwa mwingine anaweza akamwamba hana alichoombwa lakini akakupa wewe kama pesa na vitu vingine.

9. Anachukulia matatizo yako kama ni yake.

Unapomueleza kuwa ana tatizo anajali tatizo lako kama vile ni lake na hujisikia vibaya sana na kuhuzunika na atafanya lolote ili aweze kukusaidia utoke katika hilo tatizo.

10.  Mikwaruzano ikitokea katika urafiki wenu hayupo tayari kukupoteza kabla hajakuambia anakupenda.

Kwa kuwa anakupenda endapo ikatokea mikwaruzano basi atafanya juu chini kuyaweka mambo sawa ili asikukose

11. Mnapoongea:

Sikiliza sauti yake,kama anaona aibu sauti yake itakuwa ya upole/laini.
anaweza akaanza kushika shika nywele zake au kuweka sawa mavazi yake.
Hawezi akakuangalia machoni atakuwa anakuangalia kwa kuibia.
Msichana anayekupenda anakuwa na tabasamu unapoongea naye kama amekuzoea,
ila kama hajakuzoea anapokuona gafla tabasamu hutoweka maana anakuwa na aibu.

12. Anapenda hugs na kukushika:

Unapotembea naye mahali anapenda kushika mkono wako,au unapokutana naye
anaweza kuhug.

13. Ajali za kijitakia

anaweza akaona kitu kidogo tu au mdudu halafu anakurukia,au anakukumbatia.
anaweza akatafuta sababu yoyote ilimradi tu akushike,atajitahidi usigundue
mbinu zake kwa kupotezea "Ooh i'm sorry i didn't mean it"

14. Anaibia kukuchunguza:

Unapokuwa umetulia zako unakuta anakuangalia kwa kuibia,ukigeuka anajifanya yuko busy na mambo yake kumbe anakuchunguza taratibu

15. Wangalie marafiki zake.

Anapokuwa na marafiki zake akikuona anaweza akajitenga,hata kama mmeenda out pamoja na marafiki zake utakuta yupo karibu na wewe,akiwa na marafiki zake halafu mkakutana gafla atakufuata halafu waangalie marafiki zake utakuta kama wanateta,ukiona hali hiyo kuna siri yao yeye na marafiki zake
kuhusu wewe

16. Anapenda umjali.

Anapokuwa na tatizo au anajisikia vibaya lazima akuambie,mfano mmeenda mahali kukawa na baridi hata kama si baridi sana atasema anahisi baridi ili mradi umsaidie koti lako,hata kama kuna watu hawezi kuona aibu kuvaa badala yake atajisikia vizuri anapovaa koti lako.

17. Hawezi kuzuia tabasamu.

Unapomwonyeshea tabasamu lazima na yeye akuonyeshee,hata kama kuna kitu kimemwudhi atakuonyeshea tabasamu ili mradi aonyeshe umemkuta katika hali ya furaha.

18. Ishara za mwili.

Anapopita mbele yako anaweza akafanya madoido mengi ambayo yatakuvutia ila kama anajiamini.
kama hajiamini anapokuona gafla anakosa amani,utamwona anashtuka gafla.

19. Anafurahishwa na vituko vyako.

Huwezi ukamboa,hata kama ukifanya kituko ambayo haichekeshi utakuta anafurahia.

20. Anakujali:

Anakuwa anakujali,mfano akiona umeumia labda umejigonga,yupo radhi akuhudumie.Unapokuwa naye anaweza kuuliza…"unahitaji chochote?….unaweza ukasema "nina kiu ngoja ninunue maji" utamsikia "nina maji,kunywa haya yangu kwanza".basi ujue kwamba anakujali.

NB:Kama hujampenda unaweza ukajiepusha naye hatua za mwanzo ili msiende mbali na kuingia kwenye mahusiano ya kumwumiza hapo baadaye,Wengine wanaweza kufanyiwa hizo ishara zote na wasiweze kugundua,Cha msingi unatakiwa uwe na mda wa kumsoma mpaka pale atakapokuzoea kabisa na akaanza kushindwa kuficha hisia zake,siyo rahisi kwa wanawake wengi kumwambia mwanaume direct kuwa anampenda,baada ya kuona dalili zote unaweza kumtongoza na kumtamkia unampendautakuwa umemrahisishia kazi.