February 12, 2018

Una harufu mbaya na weusi kwenye kwapa? fanya hivi kujitibu.

Weusi kwapani sio ugonjwa unaoweza kutibika kwa dawa za hospitali. Mara nyingi hali hii husababishwa na matumizi ya kemikali kwapani wakati wa kujisafisha. Kukaa kwa muda mrefu na seli zilizokufa kwapani na kutumia manukato au ‘deodorants’ kali kupita kiasi.

Inapotokea mtu akiwa na hali hiyo hujikuta akikosa raha na hata kushindwa kuvaa nguo ambazo zinaweza kuacha wazi sehemu hiyo ya mwili wake.

Kama nilivyotangulia kueleza hapo awali, tatizo hili halitibiwi na dawa za hospitali. Zipo njia za asili ambazo zikifuatwa kwa usahihi, ni tiba tosha.

Limao ni tiba mojawapo ya tatizo hili. Virutubisho vilivyomo ndani ya limao vina uwezo wa kuua backteria wanaosababisha weusi na harufu mbaya kwapani, sambamba na kuondoa seli zilizokufa.

Njia nyingine inayoweza kukabiliana na tatizo hili ni matumizi ya mafuta ya nazi. Vitamin E iliyopo kwenye mafuta haya husaidia kung’arisha kwapa na inaweza kutumika kama ‘deodorant’ pia.

Tiba hii inaweza kutumika baada ya kusafisha kwapa na kuhakikisha limekauka kabisa. Chukua mafuta ya nazi na upake ukisugua eneo lote lenye weusi na uache kwa dakika zisizopungua 20.
ili kupata matokeo mazuri, ni vyema ukachagua njia moja itakayokufaa ambayo ndiyo utakuwa unaitumia kila mara, kuliko kuchanganya zote kwa pamoja.