February 11, 2018

Vitu (20) ambavyo kizazi cha sasa hivi hawawezi kufanya/kuvikosa

 
1. Kupakwa GV kwenye kidonda

2. Kung'olewa jino kwa uzi

3. Ubwabwa kupikwa jumapili tu

4. Kidonda kuwekwa unga wa 'rangi mbili' a.k.a tetesakrin

5. Kupamba kadi na pamba sebuleni

6. Ukumbi wa sherehe kupambwa kwa toilet paper

7. Kunyolewa kwa mkasi

8. Kufunga pesa kwenye leso au pindo la kanga

9. Wavulana kuvaa nguo ya ndani aina moja nchi nzima (VIP), usiombe ikakatika ukakuta imebana kifua.

10. Ku rewind kanda kwa peni

11. Nchi nzima Kuangalia Movie ya Commando John, Double Impact, Rambo na Bruce Lee..

12. Watoto Wa Mtaa Mzima Kufahamiana sababu ya kucheza Wote Jioni Kombolela na Kibaba..

13. Kuunguzana na tunda ya Ubuyu baada ya kulisugua chini

14. Kukata ndala, ati ni kifutio

15. Kunyolewa msalaba shuleni kisa nywele ndefu

16. Kuweka Vibox box kwenye Shati la shule Mgongoni..draft

17. Kuweka Shati la Shule "Blue" eti liwe maridadi.

18. Ubitozi Ulikuwa ni Kusimamisha Kola Ya Shati.

19. Ukiandika Barua kwa Umpendae lazima uchore moyo na Mkuki na lazima upulizie Pafyumu ya "YU".

20. Hata kama Mlikuwa mmegombana January lakini Mtu anakuambia "Utaipata Siku Ya Kufunga Shule".

Je wewe unakumbuka nini?? acha comment yako tujikumbushie Enzi hizo.