March 13, 2018

Acha uongo mahusiano yenu yadumu.

Kamwe usianze mahusiano yako kwa kusema uongo, ipo siku uliyoyaficha yatagundulika, yamkini ulimficha mwenzako juu ya umri, kipato, uwezo kifedha, hali ya ndugu, kiwango cha elimu,
makazi yako, kazi yako, uwezo wa familia, mahusiano yako ya awali, kuwa au kutokuwa na mtoto, kuwahi au kutowahi kuoa au kuolewa N.k. Fedheha ya kuumbuka huko mbeleni ni chungu
na yenye majuto sana bora uwe mpole na ukubali kuwa mkweli mapema. Hakuna maisha magumu kama kuishi ukijitahidi ku justify ulichowahi kusema uongo. Na hiyo kweli itakuweka
HURU -