March 14, 2018

Dalili za mtu ambae hana upendo kwako.

Uyapokee nitakayokueleza, hata kama yanaumiza ni vema ukajiruhusu kuyaelewa. Si kweli kwamba yuko busy. Si kweli kwamba simu yake ni mbovu. Si kweli kwamba hua anasahau kukujibu sms zako. Si kweli kwamba kila wakati yuko mbali na simu.

Kama mawasiliano yake na yako ni ya mashaka ni kwamba hana tena kitu cha kukuambia. Kama mawasiliano ni ya kulazimisha, ni wazi kwamba hakufikirii na haupo akilini mwake tena.


Kama kila siku wewe ndio wakuanzisha mawasiliano ni kwa sababu kuna asilimia za kutosha tu za upendo zilizopungua kutoka kwake. Si kweli kwamba hana vocha, ni wazi kwamba ameamua tu kutokuwasiliana na wewe kwa sababu ameona hamna haja.

Si kweli kwamba sms yako hakuiona, na wakati ulipomtumia tu ukapata delivered report au blue tick...ni kwamba ameona kama unmsumbua ukizingatia akilini mwake wala haupo.

Kama hataki hata kukutafuta ingawa yuko active kwenye social media kama WatsApp, Instagram, facebook, etc..basi hiyo itoshe kukufahamisha kwamba kwake wewe wala sio kipaumbele kama yeye alivyo kipaumbele kwako.

Acha kujaribu kushawishi nafsi yako kwamba atakutafuta. Acha kujaribu kujiaminisha kwamba anafanya hivyo kwa nia njema. Dalili kubwa ya mtu ambae anatafuta namna ya kuvunja uhusiano sio kukueleza wazi kwamba hakupendi na hakutaki....kusema hivyo roho humsuta...dalili kubwa ni mawasiliano kupungua, mawasiliano ya kulazimisha na kusingizia ubize. Ubize gani mpaka mtu akose walau dk tano tu za kujuliana hali?

Kama mtu hawezi kufanya vitu vidogo tu mfano kukujulia hali asubuhi, kukuuliza siku yako imeendaje, kukueleza kuhusu siku yake ilivyoenda, na kukutakia usiku mwema ili utakapoenda kulala usijihisi kama hupendwi na upo mpweke, hiyo itoshe kumuacha aende..kwa sababu sicho ambacho unastahili.

My wisdom "Letting go means to come to the realization that some people are a part of your history, but not a part of your destiny."