March 25, 2018

Emoji za ulemavu kuanza kutumika hivi karibuni.

Kampuni ya Apple imepanga kutambulisha emoji mpya siku za mbeleni ambazo zitawawakilisha watu ambao wanaishi na ulemavu.

Emoji hizo zitakuwa ni pamoja na kiti cha kutembelea (wheelchair), miguu na mikono ya bandia na vinginevyo.

Kampuni hiyo imeeleza kuwa kuongeza emoji hizo ni ishara ya kuongeza uzoefu wa watu duniani kwa kuhusisha hata ambao wana ulemavu ili wawe sehemu ya mawasiliano ya aina zote.