March 26, 2018

Fanya haya kumpata umtakae katika maisha yako.

Kabla hujaanza kuzunguka huku na huko kutafuta mchumba mcha Mungu, anza leo kumcha Mungu. Haiwezekani binti au kijana unakesha baa, club na mambo kama hayo halafu Mungu akupe mwenza mcha mungu, la hasha, Mungu hawezi kumpa mtoto wake anayemcha mtu kama wewe ambaye huendi kanisani wala msikitini, huna maombi binafsi, haufuati neno la Mungu na hauna uhusiano binafsi na Mungu halafu unahitaji mcha Mungu.

Unataka mume au mke mkarimu, mpole, mwenye upendo wa kweli. Hakikisha hizo sifa unazo kwanza wewe. Jambo la kwanza la kuwa na mahusiano imara ni ku invest kwako kujenga kiroho chako, character na muonekano. Hivyo kabla hujaangalia kushoto na kulia jiangalie kwanza wewe.