March 21, 2018

Hii ndio Kompyuta ndogo zaidi duniani yazinduliwa.

Yaani katika dunia hii ya sayansi na teknolojia hakuna kitu kinachoshindikana tunachosubiri ni muda tu kuona maajabu ya wazungu.

Kampuni ya vifaa vya kielekroniki kutoka nchini Marekani IBM jana Machi 19, 2018 ipo mbioni kuzindua kompyuta ndogo zaidi kwa muonekano kuliko kopyuta yoyote hapa duniani.

Kompyuta hiyo ambayo ni ndogo sawa na punje ya mchele, IBM kupitia kwenye mkutano wao wa THINK 2018 wamesema kuwa kompyuta hiyo ina ukubwa wa saizi ya 1×1 mm na itakuwa na nguvu sawa na kompyuta zenye mfumo wa 32 bit (x86).

Hata hivyo, kompyuta hiyo itatumika zaidi kwenye kazi za mfumo wa Artificial Intelligence na kazi nyingine kama kukagua usalama wa bidhaa kutoka viwandani na kudhibiti vitendo vya wizi.

IBM wamesema kuwa kompyuta hizo zitakuwa na bei  ya kawaida na kwa wale watakaohitaji kompyuta hizo wanaweza kuweka oda kwenye website yao na watazipata baada ya miezi 18.

“Teknolojia hii itafanya usafirishaji wa bidhaa kuwa salama zaidi hususani kwa bidhaa za vyakula, Madawa, bidhaa za nafaka na uhakiki wa bidhaa feki,“amesema Mkurugenzi Mkuu wa IBM, Ginni Rometty.

Mpango wa IBM juu ya kompyuta hizo kwa miaka mitano baadaye ni kuja kutumika kwenye simu janja ili kuongeza ufanisi wa simu hizo.
                                                    Kulia ni mfano wa kompyuta hizo