March 19, 2018

Hiki ndicho ambacho mwanamke hawezi kukueleza.

Kabla ya kuanza kuainisha siri walizo nazo wanawake wengi mioyoni mwao juu ya wapenzi wao, ni vizuri kwanza nikaelezea maana ya halisi ya siri ya moyoni. Hizi ni siri za ndani, ambazo muhusika hushindwa kuzitoa kwa hofu ya kuachwa na mpenzi wake.

Hapa namaanisha kwamba hatakama kuna kitu utakacho mfanyia na hakipendi, huwa vigu sana kwake kukueleza wazi na badala yake hubaki akiumia, akisubiria muujiza wa mabadiliko yako! Wakati mwingine huamua kueleza kwa ishara ambazo wanaume waerevu huelewa na kuweka mambo sawa, lakini wale walio na uelewa hapa hubaki wakivurunda kila siku katika uhusiano wao.

Hii ni mada ndefu na muhimu sana katika maisha ya mapenzi, ila kumbuka inakuhusu sana wewe mwanaume unayesoma na kukuweka sawa hata wewe mwanamke unayeteseka na siri hizo. Baada ya kuona siri hizi ni vizuri ukamchunguza mpenzi wako na mwisho wa siku ufanye mabadiliko katika penzi lako ila kila mmoja afurahie kuwa na mwenzake. Sasa tuanze kuona siri izo.

1. Uaminifu wako kwake 

Kwa mtazamo wa kawaida unaweza usione kama hii ni siri, lakini tunapozungumzia saikologia ya uhusiano hili ni siri nzito kwa mwanamke! Wengi wanafikiri kuishia kumwambia mpenzi wako unampenda pekee inatosha kumfanya aamini kkila unachoifanya.

Hili halina ukweli hata kidogo, mwanamke anapenda uwe mwaminifu katika kiwango cha mwisho kwake, hataki kuwa na mashaka na wewe katika kila unachokifanya. Anatamani kuwa salama hata utakapo kuwa mbali naye kwa sababu za kikazi au mambo mengine.

Ili uhaminifu huo ambao mwanamke anauhitaji kwako uwepo, lazima uwe na penzi la dhati kwake, uwe huna 'kimeo' chochote nje. Kwa maana hiyo, wakati mwingine mpenzi wako atakuwahuru na simu yako. Wanaume wengi huwa wakali sana kwa simu zao, utawasikia wakisema; ''hii ni simu ya mkononi bwana, unaing'ang'ania ya nini? Sitaki kuona ukipokea simu yangu wala kusoma sms zangu!'' mh! Jamani haya ni mapenzi ya wapi.

Kuna nini cha siri ulichoficha katika simu yako? Kama ni kweli unampenda na upo huru kwake, huwezi kumzuia kushika simu yako. Kumbuka wanawake wengi ni dhahifu, huwa hawapo tayari kumpoteza mwanaume wake kwa vitu vidogo lakini ukweli ni kwamba hubaki na siri ya maumivu moyoni mwake, wakati huo huo akiwa kituoni akimsubiri mwanaume mwenye mapenzi ya kweli atakayekuwa mwaminifu kwake. Upo tayari kutoswa? Jijibu mwenyewe!

2. Uhitaji wa fedha

Wanawake wengi (hasa walio katika urafiki au uchumba) huwa wanaogopa sana kusema moja kwa moja kwamba wanahitaji fedha! Hata kama uhitaji huo ni kwa ajili ya jambo muhimu sana, lakini kwao huwa ni shida.

Naomba nieleweke katika hili, hapa namzungumzia mwanamke ambaye ana mapenzi ya kweli kwako na ndoto yake ni kuishi na wewe siku moja, hili haina maana kwamba wanawake huwa wanaogopa kuomba pesa, hapana! Kwa wale vicheche ambao wapo kwako kwa nia ya kuchuma na kuondoka, hawashindwi kukuomba pesa asubuhi, mchana na jioni kama dozi ya dawa za malaria.

Mwanamke wako ambaye anakupenda na kukuheshimu, hawezi kukuambia moja kwa moja, anahitaji fedha kwa ajili fulani, hasa kama ni kubwa. Mara nyingi atahishia kukuambia kwa mafumbo na kutumia mifano kwa watu wengine.

Mthalani utamsikia akisema; ''mh sweetie dorah amependeza sana na rasta zake za kimasai, yaani kama nigesuka vile ningependeza sana.'' kauli hiyo inatosha kabisa kukufanya uelewe kwamba, mpenzi wako anahitaji pesa ya kusukia rasta za kimasai.

Hapo unatakiwa kucheza na hisia za mpenzi wako vizuri, sio kila kitu akuambie. Upo hapo ndugu yangu?

3. Tabia ya ububu

Hii ni siri nyingine iliyojificha mioyoni mwa wanawake wengi, inawezekana kabisa hujawai kumfikisha kileleni tangu mlipoanza uhusiano wenu, lakini hawezi kukuambia. Ni kama bubu! Anajitahidi kukufanyia vitu fulani vya hapa na pale ili ugundue kuwa unachokifanya hapendi, lakini kwa sababu wewe unajifikiria peke yako inakuwa vigumu kugundua moja kwa moja kwamba mpenzi wako hajafurahishwa na wewe faragha.

Tatizo kubwa katika hili ni kwamba, wanawake wengi huonesha kufurahia sana wanapokuwa faragha na wapenzi wao kwa nia ya kukufanya usijisikie vibaya, uone kwamba kazi unaiweza, lakini moyoni mwake anaumia na anawaza kutafuta mwingine atakayeweza kuikata kiu yake ipasavyo.

Inawezekana akawa anakupenda pasipo kawaida, lakini kwa kosa hili ni rahisi sana kutafuta mwanaume mwingine ambaye hatakama hatampenda, lakini awe na uwezo wa kumfarahisha ipasavyo faragha.

4. Uwazi wa penzi lenu

Mwanamke anapenda kupendwa! Mara nyingi wanawake ndio hasa huwa na mapenzi ya dhati zaidi kuliko wanaume. Mwanamke anapokuwa na mpenzi wake, humpenda kwa moyo wake wote, hivyo hupenda kuwa salama katika penzi la dhati kwako.

Anapenda uhuru, kujisikia wazi kwako mahali popote. Mwanamke anajisikia vibaya sana anapokuwa kana uhuru hata wa kukushika mkono mnapokuwa barabarani pamoja. Anapenda penzi la uwazi!

Maana mwingine utakuta akikutana na rafiki yake, badala ya kutambulisha vizuri kama mpenzi wake, anaanza kupatwa na kigugumizi. Utamsikia akisema: ''ah! Huyu ni rafiki yangu bwana, anaitwa....'' hili ni kosa kubwa linalofanyika na wanaume wengi bila kujua wanakosea! Mwanamke anakosa amani ya moyo kutokana na unavyomtafsiria mbele ya rafiki zako.

Kidonda hiki hubaki moyoni mwa mwanamke, huwa vigumu sana kuonyesha wazi kwamba amechukia kutokana na uliyomfanyia, lakini atabaki akiugulia moyoni mwake kwa uchungu. Hata hivyo, kinachokuja akilini mwake ni kutafuta mwanaume mwingine ambaye atakuwa wazi kwake ili aweze kufurahia mapenzi badala ya kuendelea kuumia moyoni mwake.

5. Kujali kwako

Mwanamke anapenda awe pekee kwako, umsikilize, umjali na umpe kipaumbele katika kila unalolifanya. Wanawake wengi wanapenda kudekezwa, lakini hawapendi kuweka hilo wazi kwa mwanaumme. Kwa kumtazama tu utagundua mpenzi wako anahitaji nini zaidi kwako!

Wakati mwingine anaweza kukupa mitihani ili kupima kiwango cha penzi lako kwake! Anaweza kukuambia kuwa anaumwa au anauguliwa na mtu wake wa karibu sana