March 25, 2018

Huu ndio wasifu wa mwanaharakati Mange Kimambi.

Nilizaliwa Hindu Mandal, Hospital- Dar es Salaam. Cheti changu cha kuzaliwa kina mwaka tofauti na passport yangu.

According to my passport, I was born in 1980 lakini tukifuata Birth Certificate kuna difference ya 4 years. Hii imetokana na kuna wakati mama yangu alitaka kunitoa kwa baba yangu akidai kwamba nina miaka chini ya 7.

So kutokana na sheria za Tanzania natakiwa kuishi na mama. Baba yangu naye akawa na documents zake zinazosema nimeshapita miaka 7 kwa hiyo natakiwa kuishi na baba.

So mama alikuwa na cheti changu cha kuzaliwa chenye umri tofauti na baba naye na passport yangu yenye umri tofauti. GO FIGURE.

Primary nilisoma Arusha School iliyoko Arusha- the best memories of my childhood came from my time there. Nilifanikiwa kufaulu mitihani ya darasa la 7 na nilichaguliwa kujiunga na Arusha Secondary.

Baba yangu alifurahi sana na akanizawadia kwa kunipeleka kusoma Zimbambwe. So niliishi Harare miaka kadhaa kwa masomo yangu ya secondary.

Baada ya hapo nilikwenda Marekani kuanza masomo yangu ya juu. Kwa bahati nzuri (siwezi kusema bahati mbaya) nilijifungua mtoto wa kike, Bhoke, nikiwa Marekani jambo ambalo lilinifanya nirudi nyumbani kujipanga upya.

Then in 2004 nilijiunga na AVU-UDSM ambapo nilipata degree yangu ya Business Administration na sasa nipo Dubai nasoma Masters(MBA)

Mostly nimekulia Dar-es-salaam.

Mimi nimelelewa na baba yangu pamoja na mama yangu wa kambo. Baba alinipenda mno kama roho yake yote. Ila mama yangu wa kambo alinitesa sana.

Niliishi maisha machungu sana enzi za utoto wangu. Huyu mama aliolewa na baba yangu nadhani kabla hata sijafikisha miaka miwili. Imagine mwanamke ukabidhiwe mtoto wa miaka miwili huyo mtoto si atadhani wewe ni mama yake? Ila mama yangu wa kambo alikuwa na roho mbaya sana.

Alikuwa akinipiga sana, kunitukana sana, hanivalishi vizuri kama anavyowavalisha wanae. Alichokuwa akichukia zaidi ni mapenzi baba yangu aliyokuwa nayo kwangu. Ilifika stage nilikuwa nalilia kusoma boarding school ili tu niwe mbali naye.

Na kutokana na mateso niliyokuwa nayapata kwa mama yangu wa kambo, nilijikuta nimekuwa bully shuleni. Kwanza nilifukuzwa shule ya vidudu nikiwa na miaka 6 sababu ya kupiga watoto wa kihindi.

Imagine miaka 6 nilifukuzwa shule! Primary nilisoma Arusha school, ambako huko ndo mpaka leo nina maadui sababu nilikuwa ni mwonevu sana. Nilikuwa napiga sana watoto wa wengine.Nilikuwa sisikii,nilikuwa mtoto mtukutu.

Baadaye nilikuja kuelewa kuwa hii yote ilitokana na mateso niliyokuwa napewa na mama yangu wa kambo nyumbani na ndio maana na mimi nilikuwa nikifika shule nawafanya watoto wengine kama mimi navyofanywa nyumbani kwetu.

Mama yangu wa kambo alikuwa ni mnyanyasaji sana wa wafanyakazi wa ndani. Nyumbani kwetu siku zote kulikuwa na vyakula vya aina mbili; chakula chetu cha familia na chakula cha wafanyakazi. Na wafanyakazi chakula chao ni ugali maharage au ugali na mchicha. Nyama wanakula mara moja kwa wiki,na wali pia wanakula mara moja kwa wiki. Ilikuwa inaniuma sana mpaka nikaanza tabia ya kupakua chakula kingiii ambacho siwezi kumaliza ili niwape angalau waonje.

Yaani nilikuwa najiona na mimi nina hadhi kama ya wafanyakazi wetu kwa jinsi alivyokuwa akinichukia. Naamini angekuwa na uwezo hata mimi angekuwa akininyima chakula.

Leo hii ninavyoishi mimi,chakula ninachokula mimi ndicho anachokula mfanyakazi wangu. Hata siku moja sijawahi kumwambia ale tofauti na ninavyokula mimi.

Ila kwa upande mwingine yule mama kutokana na maisha magumu aliyonipa tangu nina miaka miwili mpaka nimekuwa mkubwa amenisaidia sana. Kutokana na yale mateso nilijifunza kuji-defend, nilijifunza kufight for myself na the biggest thing nilijifunza ni kwamba hata leo hii ningeolewa na mtoto mwenye mtoto asiye wa kwangu ningempenda huyo mtoto zaidi ya wa kwangu niliyemzaa.

KWA KWELI MY CHILDHOOD WAS THE WORSE PARTY OF MY LIFE, huwa sipendi hata kufikiria wala kukumbuka. Yule mwanamke aliniumiza sana, ila alisahau kwamba watu huwa wanakuja kuwa watu wazima na huwa hawasahau especially kama hujawahi hata kuomba msamaha kwa ulichofanya.

Kuhusu michezo; nilikuwa napenda michezo mingi sana. Nilipata bahati ya kwenda shule iliyokuwa inajali sana sports(Arusha School).Yani mimi ni nilikuwa kapteni wa michezo yote, swimming, kukimbia, na wakati na graduate nilipata tuzo ya sports girl of the year.

Tukio la utotoni ninalolikumbuka mpaka leo ni hili; nilisomaga Bunge Primary School kwa muda wa mwaka mmoja. Basi kuna wakati sikwenda shule kwa muda wa wiki 2 nilikuwa naenda kucheza. Baba yangu akapata taarifa siendi shule. Basi kesho yake akaenda na mimi mpaka shule, asubuhi wakati wa assembly akanichapa mbele ya shule nzima,yani viboko vya ukweli. Ilikuwa noma sana.