March 4, 2018

Jinsi ya kuwa balozi wa bidhaa, huduma ama kampuni.

Naamini unawajua brand ambassadors. 
Hawa ni mabalozi wa bidhaa ama huduma ama biashara flani. Soma makala hii ujifunze namna unavyoweza kuwa balozi wa bidhaa ama huduma ama kampuni. Balozi wa huduma, bidhaa ama kampuni huwa ni mtu ambae yupo tayari kuiongelea na kusukuma mbele kampuni, bidhaa ama huduma kwa kutumia upekee wake katika kuvutia watu.

Si kazi ya kuajiriwa
Mara nyingi balozi wa bidhaa ama kampuni ama huduma hawi muajiriwa. Hufanya kazi za ubalozi kwa makubaliano maalum.

Kabla hujawa balozi
Kabla hujawa balozi wa bidha, huduma ama kampuni flani inashauriwa uwe unaijua hiyo bidhaa, huduma ama kampuni na unaipenda pia. Itapendeza ukiwa mtumiaji mzuri wa bidhaa hiyo.

Hivyo basi inashauriwa kufanya utafiti juu ya bidhaa, huduma ama kampuni husika kabla hujafikiria kuwa balozi wa bidhaa, huduma ama kampuni hiyo.

Sifa muhimu za balozi
Ili uwe balozi mwenye mchango chanya katika kukuza mauzo ya bidhaa ama huduma na kukuza jina la kampuni ni lazima wewe mwenyewe uwe ni mtu mwenye jina. Umaarufu wako na namna unavyokubalika katika jamik ndivyo unavyoweza kuwashawishi wengi zaidi kutumia bidhaa ama huduma hiyo.

Pia lazima uwe mtu mwenye ushawishi.
Ushawishi usiwe tu wa kikomedi bali uwe ushawishi wa kihalisia. Hii ina maana uwe umewahi shauri watu na wakafanikiwa kupitia ushauri wako.

Mfano unataka kuwa balozi wa kipodozi flani. Kwanza lazima uwe unakijua vyema. Uwe umewahi kitumia. Uwe na uhakika juu ya kutokuwepo madhara kwenye kipodozi hicho.

Uwe maarufu na mwenye ushawishi. Hapo unaweza anzisha mazungumzo na watengenezaji wa kipodozi hicho juu ya uwezekano wa kukuteua kuwa balozi wao katika eneo flani. Kama kweli una uhakika kuwa ushawishi wako utawaongezea mapato watengenezaji wa kipodozi hicho basi ingia nao makubaliano ya kupata commision.

Hivyo basi ni muhimu kujijengea umaarufu chanya
Umaarufu chanya ni umaarufu usio wa skendo. Umaarufu huu hutafutwa kwa kuwekeza nguvu, maarifa, fedha na ujuzi kwa muda mrefu. Umaarufu chanya humfanya mtu kuwa na ushawishi mkubwa sana kiasi kwamba hata akisimama kwenye media na kusema kitu flani ni kizuri sana basi watu wengi wataanza kukitumia kitu hicho.

Hapa anaetaka kuwa balozi ndio humwendea mtengenezaji bidhaa
Na huwa na proposal nzuri sana ya namna ya kusukuma mauzo ya mtengeneza bidhaa na hueleza kwanini anadhani kwa umaarufu wake na ujuzi wake kuhusu hiyo bidhaa ama huduma ama kampuni utasaidia kufikia lengo hilo.

Hii ina maana kwamba pia kama unatamani kuwa balozi wa bidhaa ama huduma ama kampuni flani lazima uwe mzuri katika kuandaa proposals.