March 16, 2018

Jua mambo haya muhimu kuhusu zinaa(sex).

Wanandoa wengi na wasio wanandoa wanazini na huku mioyoni mwao wanasema tukifanya tutatubu
ni kweli utatubu na jama toba yako ni ya kweli mungu atakusamehe lkn mambo haya hayataondoka hata kama utatubu.

1. hofu ya mungu kupungua
Kwa mara ya kwanza kabla mtu ajafanya uzinzi huwa na hofu moyoni mwake kuhusu dhambi hyo na hofu hii humfanya ajilinde na kujitunza, Lakini baada ya kufanya sex ile hofu huondoka na badala yake suala la kuvua nguo linakua ni jambo la kawaida sana.

2. kumbukumbu hubaki kichwani
Ukufanya sex utatubu lakini kuna mda yale matukio yanarudia kwenye ufaham wako mara kwa mara
Kumbukumbu hizi huwa hazifutiki na ndio maana wengi hujikuta wakizini tena baada ya kutubu

3. ujasili wa kufanya huongezeka
Mtu aliefanya uzinzi ni rahisi sana zaid kurudia kufanya tena, ukweli ni kwamba lile tendo lina raha ila ubaya unakuja tu pale linapofanywa kinyume na utaratibu.
Na kwasababu ulifanya ukatubu, na haukuona madhara yoyote yaliyokupata zaid ya burudani uliyoipata hivyo unaona urudie tena kujipa raha zaid.
Lakini biblia inasema "Mshahara wa dhambi ni mauti" warumi 6:23

4. kukosa nguvu ya kujizuia
Baada ya kufanya sex, nguvu ya kujizuia usifanye tena hupungua na yamkini hufa kabisa.
Tangia hapo utakua ni mtu wa kuanguka na kusumama, kuanguka na kusimama. Unakua sawa na mji usio na ukuta, nyumba isiyo na milango, mwizi ni rahisi au sawa na gari linalotembea bila brake
Ni wachache sana waliofanya halafu wakasimma kikamilifu bila kuanguka tena hasa pindi wanapokuwa kwenye uhusiano ambao unawafanya mkutane mara kwa mara

5. kumbukumbu hubaki vuchwani mwa watu
Unapoanguka kwanye dhambi ya uzinzi na watu wakafahamu basi dhambi hyo haitafutika katika fikra za watu hata ukifa. Mpaka leo tunasoma dhambi ya daud alipozini na mke wa uria ingawa daud alitubu akasamehewa na tayari alishakufa lkn dhambi hyo bado ipo hai inaishi kwenye vichwa vyetu na mpaka kwa wajukuu zetu bado wataisoma na kuisikia dhambi hy

Hayo tuliyoyaona ni madhara ya kudumu ambayo huweka kovu katika maisha yako lisilofutika

"Mtu aziniye na mwanamke/mwanaume hana akili kabisa, afanya jambo litakalo mwangamiza nafsi yake. Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima, wala fadheha yake haitafutika" mithali 6:32-33

"Ikimbieni zinaa, kila dhambi atendayo mwanadamu ni nje ya mwiki wake, lakini yeye afanyaye zinaa hutenda juu ya mwili wake mwenyewe" 1wakorintho 6:18