March 3, 2018

Karibu nusu ya wanawake walio kwenye uhusiano wana ‘Plan B’ ya mwanaume wa kumkimbilia uhusiano ukivunjika – Utafiti

Karibu nusu ya wanawake wote wana ‘Plan B’ – kwa maana ya mwanaume ambaye wanaweza kumkimbilia kama uhusiano wao wa sasa ukienda mrama.

Utafiti uliofanywa kwa wanawake 1,000 ulibaini asilimia kubwa kati yao wana mwanaume anayesubiria bila kuchoka kusubiria uhusiano wake uliopo uanguke na yeye kupewa nafasi.

Cha kutia wasiwasi zaidi ni kuwa wanawake waliolewa wana uwezekano zaidi ya kuwa na Plan B ya chini kwa chini kuliko wale walio kwenye uhusiano tu.

Ilibainika pia kuwa Plan B anaweza kuwa rafiki wa zamani aliyewahi kuwa na hisia na mwanamke huyo. Wengine wanaweza kuwa mpenzi wake wa zamani au mume, mfanyakazi mwenzake au mtu waliyewahi kukutana kwenye sehemu kama gym nk.

Msemaji wa kampuni ya utafiti wa mtandaoni OnePoll.com alisema: Kwa utafiti kubaini kuwa karibu ya asilimia 50 ya wanawake kwenye uhusiano wana Plan B ni ishara inayotia wasiwasi.”