March 26, 2018

Kisa cha mwanamke mvivu.

Ilikua jioni ya saa kumi na moja. Alikuwa ameketi kwenye hoteli maarufu jijini akinywa kinywaji chake huku akisoma gazeti la 'The Citizen'
Muda huo huo ndipo yule slay queen anaemsumbua mara kwa mara alitokea.
"Hi handsome. Umependeza kweli. So fine I can eat you up" yule mwanamke akaongea huku akivuta kiti na kukaa karibu na jamaa.
"Nafikiri tulikubaliana kukaa mbalimbali. Nilishakwambia mimi ni mume wa mtu" Jamaa akamwambia yule mwanamke.
"Aah come on. Me siwezi nkakula nkakumaliza. Hauwezi kunikataa kirahisi hivyo, hakuna mwanaume ambae ameshawahi kunikataa". Yule mwanamke akaongea kwa kujiamini.
"Mimi ni mume wa mtu" Jamaa akasisitiza.
"Wewe ongea unavyoweza lakini punde tu ntakua na wewe. Niko bomba kuliko hata huyo mke wako".
"Huna lolote la kujifananisha na mke wangu"
"Are u sure? Kwa sura hii. Mwili na shepu hii kweli? Unaujua utamu wangu wewe. I bet mke wako hayuko vizuri kitandani kama mimi nilivyo" akamueleza huku akilegeza kidogo blouse yake kumuonesha maziwa yake yaliyotuna sawia kifuani..
"Kama ningekuwa na tamaa na sio muaminifu ungeweza kunishawishi. Ila nimekua kiakili kiasi ya kuweza kuishinda tamaa. I am a grown man, unafikiri kila ninachokiwaza ni ngono tu? Na kwa taarifa yako, namheshimu sana mke wangu..."
"Hujajaribu utamu wangu wewe. Nijaribu leo usiku huu. Twende na gari yako kwenye hotel nzuri downtown, nakuahidi kuwa na usiku mzuri ambao hutausahau..." Akamwambia huku akinyonya mdomo kumtega jamaa
"Hivi kweli unajijua wewe? Wewe ni mvivu! Mwanamke mvivu!" Akamwambia huku akimeza funda la Kinywaji chake alichokua akinywa.
"Utaniitaje mimi mvivu? Mimi ni Diva with high profile. Mwanaume yeyote atanipa chochote kunipata mimi".
"Inatosha. Je wewe unaweza kutoa chochote kutengeneza mwanaume?" Jamaa akamuuliza.
"Unamaanisha nini?" Yule mwanamke Akauliza.
"Umenikuta nikivutia na bado umemkosea adabu mwanamke ambae yuko nyuma ya huku kuvutia kwangu, unataka nimsaliti mke wangu. Mwanamke ambae yuko nyuma ya kila kitu kinachokuvutia wewe kutoka kwangu..hauko sawa wewe"..
Akachukua glasi na kumeza funda then akaendelea...
"Mke wangu ndio yuko nyuma ya kila kitu unachoniona nacho. Nilipokua na kidogo, mke wangu aliniamini na kunitia moyo. Hizi suti unazoniona nimevaa, ni idea ya mke wangu..hua namuomba ushauri wa nini cha kuvaa kila siku.
..Mafanikio yangu yamekuja kwa sababu ya maombi yake..amekua egemeo kwangu. Gari uliyoiona nikija nayo na ukaitamani tumelinunua pamoja na mke wangu.
...Naonekana navutia kwa sababu ananihudumia vizuri na ananipa amani. Unamtaka mwanaume ambae ametengenezwa kwa miaka kenda..? Nina kila haki ya kusema wewe ni mwanamke mvivu!!
Kimya.
"Nakuona ukiwakataa wanaume waliopo single wanaokuhitaji lakini unataka waume za watu, wanaume ambao wametengenezwa na wanawake wengine? Hapana. Mambo hua hayaendi hivyo. Tafuta mwanaume wako peke yako, muamini, mpe moyo, muombee, mpe support..mfanye avutie vile unatamani awe..nyie wanawake mpepewa zawadi ya kuwa na uwezo wa kulea na kubadilisha, itumie zawadi hiyo.
...Mke wangu amekua busy katika kunijenga, kamwe sitaweza kumuacha na kwenda kwa mwanamke mwingine ambae hana cha maana zaidi ya kujivunia utamu wake alionao. Hivyo basi niache tafadhali...nahitaji kwenda nyumbani nikaonane na malikia wangu. Ananihitaji na anastahili kila lililo bora.." Jamaa akaongea huku akiinuka na kumeza funda la mwisho.
Jamaa akachukua wallet yake, akafungua na kutoa Tsh 10,000 akamuwekea pale mezani.
"Elfu kumi hii jinunulie kinywaji then wakati ukinywa fikiria kuhusu maisha yako na namna gani utaacha kuwa mvivu ili upate mwanaume wako peke yako mtakaejenga nae pamoja. Mke wangu na mimi tumekulipia kinywaji.
Jamaa akaondoka huku yule slay queen akimsindikiza kwa macho.
"Sio kwa kuringa huku, na mimi nahitaji kuwa na mume wangu peke yangu" yule slay queen akajifikiria nafsini mwake!!
My wisdom "Cheating in relationship is a sign of self-regulation failure. It is a pattern indicating primitive, uncivilized inhuman behavior."