March 7, 2018

Mabilionea 25 matajiri zaidi Afrika 2017 - Forbes.

Mfanyabiashara kutoka Nigeria Aliko Dangote bado ndiye mtu tajiri zaidi barani Afrika kwa mujibu wa orodha ya mabilionea mwaka 2017 iliyoandaliwa na jarida la Forbes.

Utajiri wa Dangote unakadiriwa kuwa jumla ya $12.2 bilioni. Kuna mabilionea (wa Dola) 25 mwaka huu barani Afrika, mmoja juu ya 24 waliokuwepo mwaka jana.

Wafanyabiasha kutoka Nigeria Femi Otedola na Abdulsamad Rabiu hawakufanikiwa kuingia kwenye orodha hiyo mwaka huu.

Mtanzania Mohammed Dewji bado ndiye bilionea wa umri mdogo zaidi Afrika, utajiri wake ukikadiriwa kuwa $1.09 bilioni.

Mabilionea 25 wa Afrika mwaka 2017:

1. Aliko Dangote, Nigeria - Utajiri: $12.2 bilioni

2. Nicky Oppenheimer, Afrika Kusini - Utajiri: $7 bilioni

3. Mike Adenuga, Nigeria - Utajiri: $6.1 bilioni

4. Johann Rupert, Afrika Kusini - Utajiri: $6.3 bilioni

5. Nassef Sawiris, Misri - Utajiri: $6.2 bilioni

6. Christoffel Wiese, Afrika Kusini - Utajiri: $5.9 bilioni

7. Nathan Kirsch, Swaziland - Utajiri: $3.9 bilioni

8. Naguib Sawiris, Misri - Utajiri: $3.8 bilioni

9. Isabel dos Santos, Angola - Utajiri: $3.1 bilioni

10. Issad Rebrab, Algeria - Utajiri: $3 bilioni

11. Mohamed Mansour, Misri - Utajiri: $2.7 bilioni

12. Koos Bekker, Afrika Kusini - Utajiri: $2.1 bilioni

13. Allan Gray, Afrika Kusini - Utajiri: $1.99 bilioni

14. Othman Benjelloun, Morocco - Utajiri: $1.9 bilioni

15. Mohamed Al Fayed, Misri - Utajiri: $1.82 bilioni

16. Patrice Motsepe, Afrika Kusini - Utajiri: $1.81 bilioni

17. Yasseen Mansour, Misri - Utajiri: $1.76 bilioni

18. Folorunsho Alakija, Nigeria - Utajiri: $1.61 bilioni

19. Aziz Akhannouch, Morocco - Utajiri: $1.58 bilioni

20. Mohammed Dewji, Tanzania - Utajiri: $1.4 bilioni

21. Stephen Saad, Afrika Kusini - Utajiri: $1.21 bilioni

22. Youssef Mansour, Misri - Utajiri: $1.15 bilioni

23. Onsi Sawiris, Misri - Utajiri: $1.14 bilioni

24. Anas Sefrioui, Misri - Utajiri: $1.06 bilioni

25. Jannie Mouton, Afrika Kusini - Utajiri: $1 bilioni