March 21, 2018

Mahitaji ya aina nyumba unayotakiwa kujenga yakupasa kuzingatia yafuatayo.

1. Mahitaji muhimu katika nyumba, vyumba kulingana na familia yako,

2. Huduma ya washrooo ndani ya nyumba. Je, kuna uhakika wa maji? Kama hakuna usiweke washrooms ndani.

3. Ukubwa wa nyumba unalingana na uwezo wako? Hii imetokea mtu anakuwa na ndoto kumiliki nyumba kubwa sana let say 6 bedrooms. Anajitahi kupigana na boma lakini shida inakuja kwenye kuezeka, frems na finishing. Jenga kulingana na uwezo unavyoruhusu.

4. Ukubwa wa kiwanja. Kuna watu wanajenga nyumba kubwa wakati ana kiwanja kidogo. Huwezi hata kuzuñguka nyuma ya nyumba yako. Mwisho unakosa hata eneo la kuchimba shimo la taka, kuania nguo na watoto kukosa sehemu ya kuçheza. Mtoto yeyote hujisikia amani akicheza kwenye uwanja wao sio kwa jirani,

Ni ushauri jamani.