March 16, 2018

mambo 3 muhimu ili kuweza kuona ndoto yako inatimia.

Kitu unachotakiwa kufahamu ni kuwa, maisha ya kufanikisha ndoto/maono yako si rahisi kinamna hiyo kama unavyofikiri. Unahitaji mambo 3 ili kuweza kuona ndoto yako inatimia hasa kwenye kile kitu ulicho na shauku kubwa ya kuona mafanikio yake yakitokea maishani mwako.

1: Kujitoa kikamilifu na kupenda unachofanya (Passion)
 Ni lazima ujifunze kujitoa haswa kwenye jambo uliloamua kulifanya kila siku. Kama wewe ni mtu unayependa kuimba hakikisha unatumia muda mwingi kufanya practice ya kuimba ili kuhakikisha unaifanya sauti yako au wewe binafsi kuwa hodari kwenye uimbaji. Hivyo hivyo kwa mtu anayependa kuandika, kuchora, kucheza, nk. Usikate tamaa haraka, wekeza akili, nguvu na hata rasilimali muda kuhakikisha unajitoa kikamilifu ili kuleta matokeo kwenye hilo eneo.

2: Kuwa mtu wa kufanya jambo kwa mwendelezo na msimamo thabiti (Consistency). Acha tabia ya kufanya jambo leo kisha kesho hulifanyi tena. Hii inakupunguzia kasi ya kuwa nguri kwenye eneo uliloamua kuwekeza nguvu, akili na muda wako kulifanikisha. Watu wengi wanapenda kumfatilia mtu mwenye kujibidiisha na kuonesha kiu ya kufanya jambo kwa mwendelezo ili kufanikiwa. Ukiwa mtu wa leo nafanya kesho sifanyi unasababisha watu wasikutilie maanani kwenye kile Kitu ulichoamua kufanya.

3: Uvumilivu na subira (Perseverance). Ni ngumu kufanikisha unachokitafuta kama utakuwa na shauku ya kupitiliza ya kutaka kuona matokeo ya haraka pasipo kuendelea kufanya kile unachokifanya kwa muda mrefu. Kila jambo linahitaji uvumilivu na subira ili kukuzalia matokeo fulani unayoyahitaji. Kuwa mvumilivu kwenye ndoto yako, endelea kuweka bidii kwenye vitendo zaidi ipo siku utafanikiwa.

Believe It's Possible!