March 16, 2018

Mambo 48 muhimu kuyajua kuhusu mkeo.

1. Mkeo sio mkamilifu, msamehe.

2. Mkeo ndio uti wako wa mgongo, usiuvunje.

3. Mkeo ni tunu, mthamini.

4. Mkeo ni kito adimu, mtunze.

5. Mkeo ni rafiki yako bora, mfanye kuwa rafiki yako.

6. Mkeo ni furaha yako, mnawirishe.

7. Mkeo anatakiwa kuwa bora kabisa, mchangamkie.

8. Mkeo ni pande la mwili wako, mstawishe.

9. Mkeo sio ibilisi, usimpige teke.

10. Mkeo sio mzuri tu kitandani, mshirikishe katika kila jambo.

11. Mkeo sio adui yako, mshajiishe.

12. Mkeo sio kikaragosi, usikubali akachezewa na watu.

13. Mkeo sio hasimu wako, usishindane naye.

14. Mkeo ni mwanamke, mheshimu.

15. Mkeo sio mtu wa kawaida, usimlinganishe na wengine.

16. Mkeo sio sahani ya kunawia, usimdhalilishe.

17. Mkeo ni kama chombo laini, shughulika naye kwa uangalifu.

18. Mkeo ni malkia maridhawa, muadhimishe.

19. Mkeo sio bondia, usipigane naye.

20. Mkeo sio begi la mazoezi ya ngumi, usimpige.

21. Mkeo sio mchezo, usimchezee.

22. Mkeo anahitaji kunyegeshwa, msimbake.

23. Mkeo ni sumaku, nasa kwake.

24. Mkeo ndio gwiji wa mahabba, msifu.

25. Mkeo ni mtu muhimu, mpe taadhima.

26. Mkeo ndiye mkeo, mkubali.

27. Mkeo ndio mzinga wa asali yako, mfukuzie.

28. Mkeo anahitaji taadhima yako, usimuaibishe hadharani.

29. Mkeo sio kisu, ishi naye kwa wema.

30. Mkeo ni wa kipekee, usimdhihaki.

31. Mkeo ni mwenye kukuenzi, usimtilie shaka.

32. Mkeo sio mpumbavu, sikiliza ushauri wake.

33. Mkeo sio habithi, usimfanyie uhabithi.

34. Mkeo ndio rafiki mwenye muamana, mfanye kuwa rafikiyo.

35. Mkeo sio leso, usimtumie vibaya.

36. Mkeo sio mfanyakazi wako wa ndani, msaidie jikoni.

37. Mkeo ni mwenye ashiki, usiache kumuenzi.

38. Mkeo ni muhimu sana kwako, usimtelekeze.

39. Mkeo ni malkia muadhama, usizozane naye.

40. Mkeo ndio mmiliki wa kiti cha moyo wako, msaidie akikalie vizuri

41. Mkeo ana akili, usimshushe thamani.

42. Mkeo ni jukumu lako, mhudumie.

43. Mkeo ndio wewe mwenyewe, usimtenge kitandani.

44. Mkeo ni namba moja katika maisha yako, mpe kipaumbele.

45. Mkeo ni hazina yako, ilinde na uitunze.

46. Mkeo anahitaji usaidizi wako, msaidie.

47. Mkeo anahitaji umakini wako, usimakinike kwenye T.V

48. Mkeo ni mwenye thamani, muongezee