March 31, 2018

Mapambo ya ukumbi wa harusi, sendoff ama kitchen party. (Party 2)

Katika sherehe yoyote ile iwe harusi, sendoff, kitchen party kitu cha muhimu zaidi huwa ni steji sehemu ambapo maharusi ama wahusika wakuu wataketi pamoja na wapambe wao.

Lakini pia Steji ni sehemu ambayo iko mbele kabisa ya ukumbi na inayoonekana, macho ya ukumbi mzima yote yako stejini lazima meza na viti vyake vipangwe katika mpangilio mzuri na wa kuvutia.

Kuna namna mbalimbali za kupamba ukumbi kwa ajili ya sherehe hiyo maalum, steji ipambwe kulingana na rangi za sherehe ili zisijeonekana haziendani na sherehe

Ni jambo la muhimu sana kuchagua rangi nzuri na za kupendeza ili kuleta mvuto kwa waaalikwa wa siku hiyo  ongea na wataalamu wa upambaji kwani watakupa maelezo ya namna ya kuchagua rangi na mpangilio.

Zifuatazo ni picha mbalimbali za muonekano wa stage ya harusi, sendoff na kitchen party