March 24, 2018

Muogope mwanaume anae badilishia gia angani.

Yaani unakutana na mwanaume anakutongoza na kukupa ahadi kedekede, unatolewa outing na vijizawadi lukuki, muda wake anakupa ili tu akukamate halafu akiisha kukukamata ukawa wake wa ndoa ghafla yale yote yanatoweka halafu na wewe bado unasema una mume?

Wanawake fikeni mahala zile kitchen party  zenu mkatae kufundishwa namna ya kumkabili mwanaume wako kitandani ila pambaneni kufundishana namna ya kumtambuwa mwanaume muongo... Yaani unaingizwa mkenge na mtu ambaye anajua mtaanza lini penzi lenu na mwisho wake anaujua wakati huo wewe umejipanga kwa agano la kufa na kuzikana! Utamtambuaje muongo?

Ni kweli ni fumbo lakini mnajua kwanini mnakamtika? Wanawake mlio wengi mmejikita kutafuta mwanaume mwenye kuahidi wala hamsumbuki na mwanaume ambaye hana kitu na akasema kweli ukambeba kama alivyo, hivi unajitambua kwa thamani ya mwanamke ama ni kwa sababu wewe ni mwanamke? Thamani ya mwanamke huwezi kujilipia mahari, ila kama ni kwa sababu wewe ni mwanamke endelea kulinunua penzi kwa kujidanganya unaweza kudumu nalo ila nikwambie hata ukinuna kesho utanikumbuka, mapenzi ya kununua kwa ufupi sio endelevu! Pengine hujui kama ukimnunua mtu kwa ajili ya mapenzi ujue utakuwa mtumwa wake... Heshima ya ndoa ina matabaka mawili nayo ni mahusiano na uchumba sasa kama kwenye mahusiano wewe ndo ulijinunulia zawadi, kwenye uchumba ukajinunulia pete bado mahari ukaja kujilipia, bado haitoshi mahitaji yote kwenye ndoa na maisha yenu wewe ndo unasimamia show bado unajiita umeolewa?

Hebu tafuta shamba ukalime. Matikiti pengine funza hawatayala uje kuvuna upate mahela kuliko kupanda hela zako kwa mwanaume ambaye kwanza hajui thamani yako.