March 26, 2018

Mwanaume/mwanamke usifanye haya udumu kwenye mahusiano yako.

Unapokuwa kwenye uhusiano jitahidi kumpenda mpenzi wako kwa hali yoyote na usionyeshe dharau kwake au hata kwa marafiki zake au ndugu zake au hata wengineo. Hakuna mtu anayependa mtu mwenye dharau hata awe nani.

Na hii huwa mara nyingi inatokea pale mmojawapo kati ya wanaopendana akimzidi mwenzake uwezo iwe kwa cheo, pesa,uzuri au hata akili na mara nyingi sana inatokea kwa wasichana pale wanapokuwa wapo juu ya wapenzi wao kiuwezo.

Wasichana wanatakiwa kutambua kuwa linapokuja suala la mahusiano ya kimapenzi au ndoa uzuri sio kigezo cha pekee cha kumfanya mwanamke aolewe. Ingekuwa hivyo basi wanawake wote warembo wangekuwa ndani ya ndoa leo hii. Hii Inamaanisha kuwa hata ukiwa mzuri hutakiwi kujisahau ukaona umeshafika...Utapotea ukileta dharau kwa uzuri wako au uwezo ulionao.