March 14, 2018

Sababu kuu 2 kwanini utumie mboga za majani kwa wingi

Watu wengi tumekuwa hatuna utamaduni wa kula mboga za majani, hii ni kutokana wengi wetu hatujui  faida zitikanazo na ulaji mboga hizo.

Lakini ukweli ni kwamba ulaji wa mboga za majani ni muhimu sana katika mwili wa binadamu. Na watalaamu mbalimbali wa afya wamethibitisha ya kwamba ulaji wa mboga za majani hasa mboga zenye rangi ya kijani zina umuhimu ukubwa sana latika afya zetu.

Na miongoni mwa faida za ulaji wa mboga za majani ni kama ifuatavyo; 

1. Ulaji wa mboga za majani zinapunguza uwezekano wa kupata magonjwa sugu.
Walaji mboga mboga za kijani wana uwezekano mdogo sana wa kupata magonjwa sugu na mara kwa mara kuliko wale wanaokula nyama nyekundu kwa wingi. Endapo utakuwa na utaratibu wa kula mboga za majani mara kwa mara kuna uwezekano mkubwa wa kuzuia magonjwa yafutayo shinikizo la damu, unene, na utapia mlo.

2. Ulaji wa mboga za majani kwa wingi  ni kinga zuri dhidi ya ugongwa wa kisukari.
Tafiti zilizowahi kufanywa na watalamu wa afya walibaini ya kwamba walaji wa mboga za majani kwa wingi wanauwezekano mkubwa wa kuepuka magonjwa ya kisukuri kwa kiwango kikubwa.

Unachotakiwa kufanya ni kwamba hakikisha mboga za majani ambazo unazitumia zinakuwa katika hali ya ukijani mara baada ya kupikwa. Na wataalamu walikwenda mbali zaidi na kusema  mboga ya majani inabidi ipikwe kwa muda wa dakika tano.